‘SHILOLE’ AMCHANA UPYA ‘FROLA MVUNGI’ ADAI ‘H-BABA’ ANAMSABABISHIA ASIWE NA MAISHA MAZURI…!!



BAADA ya kutofautiana na kuwekeana bifu kwa muda mrefu, sasa msanii anayeshika kazi ndani ya bongo Shilole, ameibuka upya na kudai kuwa rafiki yake Frola Mvungi anaendelea kuwa maskini kwa sababu hataki kuachana na H-Baba ambaye hana muelekeo wowote wa maisha ingawa anafanya muziki na filamu.

Shilole na Frola Mvungi walikuwa wanaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga awali kabisa na inadaiwa kuwa Frola ndiye aliyempokea Shilole miaka kadhaa nyuma lakini walikuja kutofautiana na ndipo Mvungi alipoamua kuchukua hatua ya kumfukuza mwanadada huyo.

Shilole anadai kuwa walikuwa wakifanya misheshe wote lakini kadri siku zinavyozdi kwenda hakuna kitu ambacho mwenzake anakipata zaidi ya kukaa na kumtengemea H-Baba, kitu amacho anaamini tabia hiyo itakuja kumtokee puani mwisho wa siku.

Alidai kuwa zipo filamu kadhaa ambazo wamecheza pamoja lakini haoni mafanikio yoyote ambayo ameyapata na anahisi kila ishu anayopata huwa haifanyii kazi bila kauli ya mpenzi wake huyo ambaye anamuona kama Mungu wake kwa maisha haya ya sasa.

“Kila mtu ana maisha yake, yeye kama anahitaji kusonga mbele angeachana na huyo mpenzi wake kwani muda wote huo hakuna kitu Frola ambacho anaweza kusema anajivunia tangu alipoanzisha mahusiano na H-Baba, alisema.

Hata hivyo mwandishi wa DarTalk alipomtafuta Mvungi kuongelea ishu hii hakuweza kupatikana mpaka inaruka hewani.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter