SIKU chache baada ya mwigizaji mahiri Bongo, Aunt Ezekiel kuolewa kimyakimya, ndoa hiyo imepigwa zengwe kufuatia mwanaume muoaji kutoonekana kwenye tukio hilo.
Aunt alifunga ndoa Oktoba 18, mwaka huu na mchumba wake wa siku nyingi aitwaye Sunday Demonte lakini baada ya tukio hilo minong’ono ya chinichini ilianza huku watu wakidai kuwa, kwa namna ilivyokuwa, kuna kitu nyuma ya pazia.
“Sasa ndoa gani hii mwanaume haonekani kabisa? Au ndiyo changa la macho lenyewe? Kwa ndoa kama hizi muda si mrefu utasikia kimenuka,” alisikika akisema mmoja wa wadau walioziona picha za sherehe hiyo mtandaoni.
Aidha, kuna ambao walikwenda mbele zaidi kwa kuhoji usiri uliokuwa umetawala na hata picha ambazo zinamuonesha Aunt tu akiwa kwenye mapozi.

“Kwa ndoa ya staa kama huyu tulitarajia kuona picha za matukio mbalimbali lakini ni tofauti, kila picha ni yeye na chache akiwa na mashosti zake, mbona hatuoni za ndugu zake na tukio la kufungwa ndoa?” alihoji Husna wa Kinondoni.
Katika kushibisha habari hii, mwandishi wetu aliongea na Aunt ambaye alisema, ndoa aliyofunga wala haistahili kutiliwa shaka kwani mumewe yuko Dubai ila amewakilishwa na ndugu yake kwa kufuata taratibu za Kiislam.
“Ni ndoa halali kabisa na mume wangu amewakilishwa na ndugu yake ila ataungana nami kwenye sherehe kubwa itakayofanyika huko Dubai,” alisema Aunt.

0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....