Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri nyumbani kwa mwigizaji Aunt Ezekiel, Mwananyamala, Dar, Ijumaa iliyopita ambapo Wema na Aunt walimfanyia ‘sapraizi’ ya ‘bethidei’ Rehema ambaye ilikuwa siku yake ya kuzaliwa.
Katika hali ya kushangaza, Rehema ambaye ni shosti mkubwa wa Aunt alishtukia anamwagiwa pombe mfululizo aina ya Gordon’s na Jack Daniels huku mwigizaji Nice Chande akimmiminia chupa kubwa kadhaa za maji.
Muda mwingi Wema alikuwa akimmwagia Rehema pombe bila kushusha mkono.
Kufuatia kitendo hicho kilichoambatana na kelele nyingi za mastaa hao, kilisababisha wapita njia kujazana getini kwa Aunt bila kujua kilichokuwa kikiendelea na kudhani Rehema alikuwa akipokea kipigo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....