UTENGENEZAJI WA FAST AND FURIOUS 7 KUENDELEA BAADA YA KUSIMAMA KWA MUDA KUTOKANA NA KIFO CHA MMOJA WA MASTAA WAKE,PAUL WALKER....

Paul walker enzi za uhai wake
Utengenezaji wa filamu mpya ya Fast and Furious utaendelea licha ya kifo cha mmoja wa mastaa wake, Paul Walker. Utengenezaji wa filamu hiyo yenye bajeti kubwa ulikuwa umesimama weekend wakati wa sikukuu ya Thanksgiving ambapo Walker alipata ajali na kufa siku ya Jumamosi. Walker alikuwa arejee kuendelea na utengenezaji wa filamu hiyo jijini Atlanta nakuungana na mastaa wenzie Vin Deisel na Dwayne Johnson aka The Rock. James Wan, ambaye ni muongozaji wa filamu hiyo na wakurugenzi kutoka Universal Studios walifanya mkutano jana asubuhi kujadili jinsi ya kuendelea na Fast and Furious 7 katika njia ambayo itakuwa na heshima kwa kifo cha Walker. Kwa mujibu wa The Hollywood Reporter, kushoot kunaweza kuanza Jumanne hii. Walker alikuwa akiigiza kama Brian O'Conner, mhalifu aliyebadilika na kuwa polisi kwenye Fast and Furious 7, uhusika alioucheza katika filamu sita zilizopita za Fast and Furious. Shooting ya filamu hiyo itamalizka Januariy huko Abu Dhabi.
Fast and Furious 7 ilipangwa kutoka July 11, 2014.

PICHA ZINATISHA! MWILI WA MAREHEMU PAUL WALKER WA FAST AND FURIOUS WAONYESHWA....

.
Paul walker enzi za uhai wake



Paul Walker
Paul WalkerKwa mara ya kwanza mwili wa marehemu Paul Walker wa Fast 5 and Fast & Furious 6 umeonyeshwa kwa ulivyoonekana hapo juu

AJALI! TRENI YAUA NA WENGINE 60 KUJERUHIWA.....


Treni iliyoua watu wa nne na kuacha majeruhi 60 na change NY katika eneo la Bronx NY,  Chanzo cha ajali hii inasemekani ni speed na mbaya zaidi ilikuwa kwenye corner. Ni mtihani wa kwanza kwa Mayor mpya wa New York Bill de Blasio. Treni hii ni moja ya treni zinazojulikana kwa jina la Metro North, Metro North ni tofauti na zile  treni za ndani ya Jiji zinazofanya kazi 24/7 maarufu kwa jina la subway zinazopita chini ya ardhi. Treni za Metro North utumiwa zaidi na watu wanaoishi nje ya NY lakini ufanya kazi zao ndani ya NY. Tunashukuru hadi sasa hatujasikia kama kuna mtanzania yeyote alikuwa ndani ya treni hii kwani wapo ndugu zetu pia wanaotumia usafiri wa treni hizo za Metro North kuingia na kutoka ndani ya jiji la NY.
Wafanyakazi wa zima moto wakiwa kazini
Mayor mpya wa New York  Bill de Blasio baada ya Mayor Bloomberg.

Kati ya vitu anavyokumbana navyo Mayor mpya ni kama hivi snow ikianguka kuhakikisha inaondolewa ontime na kupunguza kero za wakazi wa jiji la wasiolala New York City. Hii ilikuwa kali ya mwaka ilitokea 2010 na kusababisha watu kutokwenda kazini kwa 2 days kwasababu ya snow kumwagika na kusababisha kutokuwa na shughuri zozote ndani ya jiji la NY.

LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA MAENDELEO YA WANAWAKE NA WATOTO MASASI,MILIONI 103 ZAPATIKANA.....

.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akizungumza wakati alipokuwa akiongoza harambee ya kuchangia maendeleo ya wanawake na watoto iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Anglikana Dayosisi Mtandi Masasi, mkoani Mtwara jana. Jumla ya Sh103 milioni zilichangishwa kwenye harambee hiyo. 
Askofu Msataafu wa Dayosisi ya Mtandi Masasi, Oscar Mnung'u akisalimu waumini.

CHADEMA WAMTAKA MSAJILI WA VYAMA KUMPUUZA NAPE

Siku moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye kumtaka Msajili wa Vyama vya Siasa kukifuta Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kushindwa kusimamia katiba yake na kutofanya uchaguzi wa ndani kwa zaidi ya miaka 10, chama hicho kimesema hakijawahi kwenda kinyume na katiba yake na kinachozungumzwa na Nnauye ni uzushi wa kisiasa unastahili kupuuzwa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa katika miaka 10 iliyopita chama chao kimefanya uchaguzi mara mbili kila baada ya miaka mitano kama katiba inavyoelekeza.

Chadema tumefanya uchaguzi mkuu wa ndani 2004 na 2009, mara baada ya kipindi cha miaka mitano kupita ya muda wa kawaida wa uongozi. Madai kwamba hatujafanya uchaguzi kipindi hicho hayana msingi,” alisema Mnyika.

“Msajili wa vyama vya siasa anapaswa kupuuza kauli hiyo ya Nape na CCM na kurejea Katiba ya Chadema ambayo ofisi yake inayo nakala yake.”Ni vyema msajili akaikemea CCM kwa kufanya siasa chafu za uongo na uzushi,” alisema.

Aliongeza: “Kauli ya Nape na CCM ni ishara ya chama hicho kutishwa na namna ambavyo Chadema kinajipanga kuanzia ngazi ya chini kujenga uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti mijini na vijijini kuanzia ngazi za chini kupitia Programu ya Chadema ni Msingi.”

Mnyika alisema Nape na CCM wanajaribu kupotosha umma unaounga mkono vuguvugu la mabadiliko (M4C) kupitia Operesheni za Kanda na kazi nyingine zinazoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamati Kuu ya Chadema itafanya mkutano wake wa kawaida kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 20 mpaka 21.

Ajenda za mkutano ni kupokea, kujadili na kufanya uamuzi mihutasari ya mikutano iliyopita na yatokanayo na mikutano hiyo, taarifa ya hali ya siasa na ripoti ya fedha.

Ajenda nyingine ni pamoja na taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba, taarifa ya utekelezaji wa Programu ya Chadema Msingi na shughuli z

Hivi ndivyo Vicheche vya Nchini vinavyofanya Laana Nyakati za usiku...


Sote  tunajua  kuwa  warembo  wa  kibongo  wa  siku  hizi  ni  balaa  kwa  kujiachia  na  kujianika  uchi ,  lakini    kiwango  chao  cha  kujiachia  ndani  ya  Afrika  Maharini  ni  sawa  na  asilimia  sifuri. ..

Mpaka  sasa  sidhani kama kuna mademu wanaoweza kushindana na warembo wa Uganda katika kujirusha, kujiachia, kula bata  na  vivazi  vya  nusu  uchi n.k. 
Kama ulikuwa unadhani wasichana wa Bongo ni vicheche,

SHOSTI UNA UHURU WA KUFUNGUKA KWA MUMEO?

 
ASALAAM alaikum/Bwana Yesu asifiwe!
Bila shaka ni wazima wa afya na mnaendelea vema na kazi zenu za kulijenga taifa, kwa wale wagonjwa nawaombea kwa Mwenyezi Mungu inshalla atawaponya na kwa waliokutwa na misiba nawaombea subra ishallah Mungu awapatie moyo wa uvumilivu.

Bila kuwachosha leo nakuja na mada nayingine mpya kwenu mashosti wangu ambao mnajifanya mabubu, hamuwezi kufunguka kwa waume zenu hasa mnapokuwa na haja za kimwili.
Shosti kufunguka kwa mumeo kunaleta mapenzi mazito sijui kama mnaelewa kufunguka huko ni  kwa aina gani? Si kwa makosa ee bibie.

Halooo sasa nikueleze tu. Wanawake wameumbwa na haya lakini kwa mumeo hakuna hilo unatakiwa kumwambia mzee nahitaji mambo na ukamuanza mwenyewe usisubiri kuanzwa.
Wewe siku zote kumbuka mume naye anachoka na ataona huna mapenzi naye kwa sababu wahitaji ni wote wawili.

Unataka kuniambia shosti hakuna siku wewe unamhitaji mumeo kwamba ni yeye tu kila siku akuanze?  Sasa wewe bubu nakufundisha kwa njia hii funguka, mueleze mumeo na umuachie mwili atalii kama atakuwa bado hajakukosha mweleze wazi ni wapi akipita anakukosha. Hii inaleta mahaba zaidi, vunja ukimya bibi!
Utakuta mke anaona aibu hata kuchojoa mavazi yake basi mwambie akusaidie kwa sababu nayo ina hamasa yake, mume kuitoa mojamoja mpaka ile ya mwisho muhimu hapo ndipo mahaba yanapoanzia na kuamsha mashamshamu.
Gizani haipendezi, acha mataa yawake kama vile kuna sherehe ili uweze kuiona kila nukta ya mumeo naye aione kila pembe ya mwili wako. Kama hupendi mwanga mkali tumia mwanga hafifu au mishumaa lakini inapendeza zaidi kuujua mwili wa mumeo au mumeo kuujua wako kwa kuuona live si kwa kuhisi gizani. Acheni woga ambao hauna maana mashosti wangu.
Unampapasaje mpenzi/mume/mke kama vile umepoteza kitu kwa sababu ya giza? Huwezi kutambua uzuri aliona mwenza wako kamwe utaishia kumsifia kwa uongo tu.
Sasa basi funguka na uwe huru kwa mwenza wako na uongeze ujuzi muhimu, unaweza kutumia macho, kidevu masikio na pua. Jitume bibi

PHOTOS:DIAMOND NDIO MTANZANIA PEKEE ALIYE ALIKWA NA P-SQUARE KUSHUHUDIA ARUSI YA PETER OKEYO

  Pichani ni Diamond Platnumz msanii kutoka bongo akiwa na bwana harusi Peter wa Psquare pale walipokutana huko Lagos Nigeria kwenye harusi ya Peter. Diamond yupo nchini Naija kwaajili ya utengenezaji wa video yake mpya ya wimbo Number One remix aliyomshirikisha msanii kutoka huko huko Naija anaitwa Davido. Nadhani tutegemee mambo mazuri sana kutoka kwa Diamond
Akiwa na Mwanamuzi Iyana

Akiwa na Adebayo wa Man City

Makamu wa Rais Dr. Bilal awaoongoza wananchi kuuaga mwili wa Dr. Sengondo Mvungi jijini Da es Salaam leo


Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt.Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo kwa ajili ya kuagwa
 Jeneza likipelekwa sehemu iliyoandaliwa
 Mashada ya maua na picha ya marehemu
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi za serikali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Sinde Warionba akiongea machache wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

 Makamu wa Rais Dkt Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 
Misa wakati wa shughuli hiyo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.

BAADA YA FILAMU ZAO KUBUMA SOKONI...BONGO MUVI SASA WASHIKANA UCHAWI...!!

Tuhuma ya mastaa Bongo kujihusisha na mambo ya ulozi au uchawi imeibuliwa upya na safari hii bundi kajikita zaidi kwenye kiwanda cha sinema za Kibongo, Ijumaa lina ripoti kamili.
http://4.bp.blogspot.com/-6rq5Op4EJJk/TvHoS15grOI/AAAAAAAACVA/0DnQiFtM1BY/s1600/26.jpg
UCHUNGUZI
Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya ulimwengu wa mastaa hao ulibaini kwamba, ukiwaacha wale wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakishikana uchawi kila kukicha, kwenye filamu ndiko hakufai.

Ilibumburuka kwamba masuala ya kurogana ndiyo yamesababisha filamu za baadhi yao kudoda na kukosa soko.
Inaelezwa kwamba mbali na sinema  zao kubuma sokoni pia wamekuwa wakizibiana riziki za tenda kama ilivyokuwa zamani.

Elizabeth Michael 'Lulu'.
KIVIPI?
Kwa mujibu wa ‘mtaalam’ wao mwenye kituo cha kazi huko Yombo-Buza, Dar, wanachokifanya ni kufifisha na kuzimana nyota hivyo kumpotezea mhusika mvuto kwenye jamii.
“Unajua kuna mastaa ambao walikuwa na majina makubwa sana lakini siku hizi siyo kama zamani.

“Baadhi wanawaroga wenzao kwa kuwasababishia matatizo ya magonjwa au kwenye familia,” alisema mmoja wa wasanii waliokuwa waking’ara zamani lakini siku hizi kafifia huku akimtolea mfano mwigizaji mmoja wa kiume ambaye mkewe aliwahi kumkuta na hirizi.
Katika uchunguzi huo, baadhi ya mastaa walikuwa wakinyoosheana vidole wao kwa wao huku listi ndefu ya mastaa wanaokesha kwa waganga kuwamaliza wenzao ikianikwa (majina tunayo).
Ili kupata uthibitisho wa uchunguzi huo, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya vinara wa filamu za Kibongo ambapo wengi walikiri kukithiri kwa ushirikina kwenye tasnia hiyo.

JACOB STEVEN ‘JB’: Sanaa yoyote ili idumu muda mrefu inahitaji baraka na neema ya Mungu. Sisi tulianza enzi za Nyota Ensemble ‘Mambo Hayo’, baadaye ilikuja Kaole Sanaa Group ndipo kukaibuka mapinduzi sisi tukashuka.
Mimi siamini mambo ya uchawi ila naamini katika kazi tu, wasanii waache kufanya kazi kimazoea.

Masuala ya kurogana mimi spendi kuyapa nafasi maana hayo kila sehemu yapo, ninachoweza kusema ni kwamba wasanii wengi wa Bongo hawapo ‘siriasi’. JACQUELINE WOLPER: Mimi naamini sana katika kazi lakini kwa kuwa Mungu ndiye kanipa jina hili, sina budi kumshukuru yeye ila kama nimelipata kwa njia ya uganga basi nikose kabisa.
ROSE NDAUKA: Uchawi ni ishu inayonisikitisha sana na ukweli wapo mastaa wanafanya mambo hayo ili wapande. Mimi najua Mungu hawezi kuwasaidia so nawashauri wafanye kazi, wasihangaike na uchawi kwa sababu hauwezi kuwapandisha.
KAJALA MASANJA: Kusema kweli uchawi unatajwa sana kwenye tasnia ya filamu Bongo hadi inanifanya kuamini hivyo kwa sababu kuna watu kweli wakikuona unang’ara kwenye muvi watafanya kila wawezavyo ili wakushushe tu na hasa kwa njia ya ushirikina.
SINGLE MTAMBALIKE ‘RICHIE’: Mimi asili yangu ni Mwanza so kama ujuavyo watu wa Mwanza ni wachapa kazi, so nipo makini sana na kazi yangu ya filamu na nipo kwenye tasnia kwa miaka 17 na maisha yangu nayafanya ya kawaida tu wala sipendi kujikweza sana.
Kwa staili hiyo ningetumia nguvu za giza ningekuwa tajiri namba moja  hapa nchini maana siri ya kazi yoyote ni kuiheshimu na kujibidiisha. ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’: Tasnia yetu ya filamu naona kama hatuangalii mbali maana kwa wenzetu wanashindana kikazi na si uchawi kama huku wanaofikiria kuwashusha wenzao kisa wanaona wanafanya vyema, mimi ninachoweza kusema watu wafanye kazi na wasibaki kuangalia nani anafanya nini na kumfanyia mambo kama hayo yasiojenga maisha.
RUTH SUKA ‘MAINDA’: Mimi sijui sana kama kuna watu wanafanya ushirikina. Ninachowaomba wamtegemee sana Mungu kwani ninachoamini mimi kila kitu kipo kwa makusudi ya Mungu. Kama ukimroga mwenzio ili ashuke basi hata wewe huwezi kufika mbali.
JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’: Kweli mimi ninaumizwa sana na watu wanaotumia uchawi kuzima nyota yangu kwa sababu kweli wapo wanaofanya hivyo tunawaona hata huko lokesheni wanakamatwa na hirizi.
Wengine wanakutwa na matunguri ila mwisho wa siku naomba wajue kuwa nyota na mafanikio ya mtu huletwa na Mungu na kujibidisha katika kazi hivyo ninachoweza kuwashauri watu kama hao waachane na imani za kishirikina.
SALUM HAJI ‘MBOTO’: Mimi ninachojua watu wanatengeneza muvi kupitia migongo ya wenzao, unakuta mtu anatengeneza sinema lakini anajua kabisa bila kumchezesha fulani hawezi kuuza hivyo anatumia nyota ya mwenzake kuuza filamu yake.
AUNT EZEKIEL: Siamini sana katika kurogana ila wanotumia njia hizo siamini kama wanafanikiwa kiasi hicho maana uigizaji ni kipaji kutoka kwa Mungu na hakuna awezae kushusha kipaji hicho ila najua uchawi upo na watu wanatumia uchawi kwenye mambo yao.
STEVE NYERERE: Uchawi haupo kwenye filamu tu hayo yapo hata kwenye siasa. Watu kibao wanatembelea nyota za watu. Wapo wanaoshinda kwa waganga, tunawajua ila cha msingi wafahamu kuwa hata ukimfanyia mtu kitu gani huwezi kuwa staa.
SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’: Mimi ninaona kama chalenji tu na kinyongo, maana wengi wanaotumia nguvu za giza hawachukui muda mrefu wanashuka wao. Ninachoona mimi waachane na nguvu za giza wamtegemee Mungu.
Baadhi ya waigizaji wengine waliowahi kurogwa na wenzao ni pamoja na Wema Sepetu, Blandina Chagula ‘Johari’, Nuru Nassor ‘Nora’ na wengineo.

CREDIT: GPL

CHANGUDOA AKIRI KUWA AMECHOSHWA NA UTUMWA WA NGONO..!

INAWEZEKANA umeshalizwa na mengi, umesikitishwa na vingi lakini stori ya dada Aziza Athumani (21), anayefanya biashara ya kuuza mwili wake, inatia uchungu sana
Aziza anayefanya biashara ya kujiuza jijini Dar es Salaam kwa sasa ni mgonjwa lakini analazimika kuendelea na biashara hiyo ili aweze kujikimu.

Sasa, hebu fuatilia mahojiano yetu na Aziza.
Ijumaa: Hebu tuambie...ni nini hasa kilikusukuma kuingia kwenye biashara hii haramu?
Aziza: Maisha kaka yangu, maisha. Nilizaliwa Mtwara miaka 21 iliyopita. Niliishi na mama na wadogo zangu. Baba yangu anaishi hapa Dar. Bahati mbaya,  baadaye mama alifariki dunia. Hapo ndipo maisha yalipoanza kuwa magumu.
Ijumaa: Kwa hiyo shughuli ya kujiuza ulianza hukohuko Mtwara?
Aziza: Hapana. Maisha yalivyokuwa magumu baada ya mama kufariki, niliamua kuja Dar kutafuta maisha. Nilifikia kwenye baa moja iliyopo Sinza, nakumbuka ilikuwa mwaka 2010, nikiwa na miaka 17. Kipato kilikuwa kidogo sana lakini wateja walikuwa wakiniachia chenji ndogondogo.
Ijumaa: Kwa siku ulikuwa unaweza kuingiza shilingi ngapi?
Aziza: Hadi 10,000 nilikuwa nafikisha, wakati mwingine inazidi kidogo. Tatizo wanaume wa baa siyo wastaarabu. Wakilewa wanaanza kukushikashika. Mimi nilikuwa mdogo kwa hiyo nilivyokataa, nilifokewa na meneja. Nikawa nawaachia.
Siku moja, mteja mmoja akanitaka, nikakataa. Ikawa kama wameambiana. Karibu wote waliokuwa wakiniachia chenji wakanitongoza, wote nikawakataa, kuanzia hapo wakawa hawaniachii chenji tena. Maisha yakabadilika.
Ijumaa: Yakawaje?
Aziza: Nikawa sina fedha za kutosha kujikimu mimi na wadogo zangu. Wakati mwingine nilikuwa nalala mwenyewe geto (chumbani), wenzangu wote waliondoka na wateja (kulala nao kwa kujiuza). Nikiwaomba pesa, wananicheka, wakaniambia na mimi nitoke. Nikajaribu...kumbe nilikuwa naingia kwenye moto (analia)...nikajikuta nimezoea mchezo wa kujiuza.
Ijumaa: Usilie tafadhali, tulia. Baada ya hapo ikawaje sasa?
Aziza: Niliona biashara ya kujiuza inalipa zaidi kwa hiyo nikaamua kuachana na baa na kujikita moja kwa moja kwenye uchangudoa. Siamini kama mimi ni changudoa lakini sitaki kabisa hii kazi, ni shida tu kaka.
Ijumaa: Pole sana...vipi kuhusu baba yako? Halafu huo mguu una tatizo gani? Pia unaweza kueleza kidogo kuhusu elimu yako?
Aziza: (analia sana – zilipita dakika tano akiendelea kulia. Juhudi za kumbembeleza zilizaa matunda baada ya muda huo).
Ijumaa: Najua inauma sana. Jipe moyo. Unaweza kuendelea sasa!
Aziza: (anafuta machozi) Huyo baba...mzee Athumani ndiyo chanzo cha matatizo haya yote! Mimi sijasoma, niliishia darasa la saba tu. Lakini nikasema nitajitahidi angalau niwasomeshe wadogo zangu ndiyo maana nikaja mjini na kujikuta nimeishia kwenye biashara ya kujiuza.
Kuna tukio ambalo siwezi kulisahau. Ilikuwa Jumamosi, saa 9 usiku, mwezi wa saba, mwaka 2011. Mimi na rafiki yangu Asha tulikuwa tumetoka kujiuza Kinondoni. Tulikodisha pikipiki moja, tukapanda kwa mtindo wa mshikaki. Kwa bahati mbaya, tulipofika Magomeni tukapata ajali mbaya. Asha na dereva walikufa palepale...Mungu amrehemu rafiki yangu Asha (analia tena...).
Nikapelekwa Muhimbili, Kitengo cha Mifupa (MOI), nikalazwa kwa siku kadhaa. Mguu wangu ulikuwa umeharibika sana na hivi unavyoona nina vyuma. Niliporuhusiwa hospitalini, nikaenda kwa baba yangu mzee Athumani, Tandika. Cha ajabu, aliponiona nina magongo, akanifukuza akisema, eti mimi siyo mwanaye. Nililia sana, lakini kwa sababu nilikuwa na akiba kidogo nikaamua kurudi nyumbani kwangu Tandale nilipopanga chumba kimoja.
Pesa ilivyoisha, nikalazimika kurudi tena mtaani kujiuza na hii hali yangu ya magongo. Maisha haya! Sijui kwa nini inakuwa hivi jamani!
Ijumaa: Pole sana dada. Hebu tuambie...unakutana na changamoto gani katika kazi yako?
Aziza: Nyingi lakini kubwa ambayo sitaweza kuisahau ni kubakwa na wanaume watatu kwa mpigo, tena nikiwa na magongo yangu. Iliniuma sana. Wanadamu wana roho mbaya sana. Nilikutana na kaka mmoja, tukakubaliana angenipa shilingi 5,000 kwa muda mfupi.
Akasema, hana pesa ya kwenda gesti hivyo tukaenda kwenye Uwanja wa Urafiki, Shekilango. Nikashangaa nimekutana na wenzake wawili, nilipokataa, walinitolea kisu, ikabidi nikubali tu. Niliumia sana siku hiyo (analia – waandishi wanambembeleza).
Tukio lingine ni pale nilipokutana na mwanaume mmoja mwenye asili ya India, akanidanganya na kuniambia nimzalie mtoto, nikabeba mimba yake. Akanikana.
Huwezi amini kaka zangu, hapa nina mtoto mdogo, hata miaka miwili hajafikisha na nilianza kutoka na kuendelea kujiuza, mtoto akiwa na miezi mitatu tu. Mungu anamnusuru mwanangu, anaendelea vizuri.
Ijumaa: Kwahiyo kwa sasa unafikiri nini juu ya changamoto hizi za maisha yako? Bado unaendelea na shughuli hii?
Aziza: Uongo dhambi kaka, bado najiuza lakini nikipata mtaji wa biashara na matibabu nitaacha. Natakiwa kurudi tena MOI mwezi wa pili mwakani kwa ajili ya kuondolewa vyuma, nimeambiwa niende na laki tatu.
Kama umeguswa na kisa cha Aziza na unataka kumsaidia kwa hali na mali, wasiliana naye moja kwa moja kwa namba 0714 021105.

-Gazeti la ijumaa

"MHE. KAPUYA HANA KOSA LA KUJIBU KABISA"...KOVA

 
Akiongea na wanahabari leo mchana kamanda kova kasema hawawezi kumuita Mhe. Kapuya kasababu haya ni mambo yake binafsi na hakuna mtu yeyote ambaye amakuja hapa polisi kulalamika kutendewa vibaya na Mhe. Kapuya.

"hata hivyo kamanda kova kasema kama kuna ushahidi wowote wa kueleweka sio kusingizia mtu vituo vya polisi viko wazi masaa 24"


 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter