|
Paul walker enzi za uhai wake |
Utengenezaji wa filamu mpya ya Fast and Furious utaendelea licha
ya kifo cha mmoja wa mastaa wake, Paul Walker. Utengenezaji wa filamu
hiyo yenye bajeti kubwa ulikuwa umesimama weekend wakati wa sikukuu ya
Thanksgiving ambapo Walker alipata ajali na kufa siku ya Jumamosi. Walker
alikuwa arejee kuendelea na utengenezaji wa filamu hiyo jijini Atlanta
nakuungana na mastaa wenzie Vin Deisel na Dwayne Johnson aka The Rock. James
Wan, ambaye ni muongozaji wa filamu hiyo na wakurugenzi kutoka
Universal Studios walifanya mkutano jana asubuhi kujadili jinsi ya
kuendelea na Fast and Furious 7 katika njia ambayo itakuwa na heshima
kwa kifo cha Walker. Kwa mujibu wa The Hollywood
Reporter, kushoot kunaweza kuanza Jumanne hii. Walker alikuwa akiigiza
kama Brian O'Conner, mhalifu aliyebadilika na kuwa polisi kwenye Fast
and Furious 7, uhusika alioucheza katika filamu sita zilizopita za Fast
and Furious. Shooting ya filamu hiyo itamalizka Januariy huko Abu Dhabi.
Fast and Furious 7 ilipangwa kutoka July 11, 2014.
'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....