Meneja wa mwigizaji huyo, Martin Kadinda
ameliambia Mwananchi kuwa ingekuwa vizuri zaidi kama washabiki na
wapenzi wa burudani kwa jumla wakashirikiana naye katika kumpa sapoti
mwigizaji huyo.
“Wema anapitia kipindi kigumu sana, nafikiri kila
mmoja wetu anaelewa uchungu wa kufiwa na mzazi. Naomba kwa niaba yake
tuungane pamoja kumfariji yeye na familia yake ili waweze kupita salama
katika kipindi hiki”, anasema Martin.
Baba wa Wema Sepetu Balozi Isaac Abraham Sepetu
alifariki dunia Jumapili wiki iliyopita katika Hospitali ya TMJ
alikokuwa akitibiwa ugonjwa wa kisukari pamoja kiharusi.
Balozi Sepetu alizikwa siku ya Jumatano Oktoba 30, 2013 kijiji cha Mbuzini, Mjini Magharibi Unguja.
Mwanamuziki Diamond ni kati ya walioshiriki msiba
wa baba Wema, hali iliyosababisha baadhi ya watu kujiuliza kama wawili
hao ambao waliwahi kuwa na uhusiano, wanarudiana au aliamua tu kuja kama
walivyo watu wengine.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....