Msichana mmoja, Mariam Chacha, mkazi wa Mtaa wa Nyasho A, mjini Musoma
amemwagiwa maji ya moto na kuunguzwa mwili, hali iliyofanywa alazwe
katika hospitali ya mkoa.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa mbili
usiku ambapo inadaiwa aliyefanya kitendo hicho ni Pendo Wambura ambaye
amekamatwa na polisi.
Habari kutoka ndani ya kituo cha polisi mjini hapa zinadai kuwa mara
baada ya Mariam kumwagiwa maji ya moto na mwenzake na kuungua sehemu za
kitovu mpaka usoni, matiti na mikono na akiwa hajitambui mpaka
sasa,wasamaria wema walimpeleka polisi ili kupata hati ya matibabu (PF
3) na akaenda kutibiwa katika Hospitali ya Serikali ya Musoma alikolazwa
wodi namba nne.
“Polisi tulikwenda kumkamata mtuhumiwa na tunamshikilia kwa kuwa
majeruhi hali yake ni mbaya, kalazwa, na tayari amefunguliwa jalada
namba MUS/IR/5009/013,” alisema afisa mmoja wa polisi kwa sharti la
kutoandikwa jina lake kwa kuwa siyo msemaji.
Shuhuda mmoja alimwambia mwandishi wetu kwamba Mariam alikwenda
kuwasalimia ndugu zake pamoja na mama yake ambaye ni mgonjwa wanaokaa
nyumba moja na mtuhumiwa.
“Mariam alipoona hali ya mama yake alianza kulia ndipo Pendo
alipokwenda kuchukua maji yaliyokuwa yakichemka ili yapikiwe ugali wa
mama mwenye nyumba na akamwagia mwenzake akidai eti anachukizwa na
kitendo chake cha kumlilia mgonjwa wake,” kilisema chanzo.
-GPL
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....