Niliwahi
kuuliza kwa watu wa nguvu shilingi milioni 75 wakipata watatumia kwenye
nini?, majibu ya wengi yalikua ni kujenga nyumba na kununua gari huku
wengine wakisema watawekeza kwenye biashara.
Sasa
basi, pamoja na hiyo milioni 75 kuonekana inaweza kufikiriwa kufanya
mambo hayo makubwa ya kimaisha… imefahamika kiwango hicho cha pesa
kinaweza kuishia kwenye kununua TV moja tu hii mpya ya Samsung ya inch
85 na usirudishiwe chenchi.
tovuti
hii ilipotembelea duka lao Mlimani City, imeambiwa TV hii ina vitu
vingi vya kipekee ikiwemo kutumia ishara ya mkono, sauti, na sura
kufanya setting mbalimbali ikiwemo kupunguza sauti badala ya kutumia
remote.
Smart
contents mfano Instagram, twitter, facebook na apps nyingine mbalimbali
ambapo unaweza kutumia Internet kuwasiliana kwenye mitandao mbalimbali
kama vile skype ambapo mnaweza kuonana zaidi ya watu watatu kwa wakati
mmoja.
Ina music system
yenye mziki mzito hapohapo hivyo ukiwa nayo huna haja ya kununua home
theatre, pia faster speed squad core processor.
Digital
tuner unaweza kupata local free channels zaidi ya 40 bila decorder na
ukitaka channel za kulipia utatumia smart card ambayo unaiweka kwenye
smart card slot nyuma ya TV yako.
Vilevile ukiwa na samsung smart phone unaweza kuiunganisha na TV ukaplay videos, music video games kutoka kwenye simu yako.
Source: Millard Ayo
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....