"NISIPIGE PICHA NIKAWEKA MITANDAO YA KIJAMII,TAYARI WATU WANASEMA...NIACHENI JAMANI,NAMI PIA NI BINADAMU" WASTARA



Wastara Juma.
MSANII wa kike katika filamu za Kibongo, Wastara Juma amewashukia watu wanaotafsiri kila kitu anachokifanya katika maisha yake na kusema: “Yaani nisipige picha nikaweka kwenye mitandao ya kijamii, tayari watu wanasema yao...jamani nami pia ni binadamu.”
Wastara ambaye ni mjane wa marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ameliambia gazeti hili wikiendi iliyopita kuwa, baada ya kuachwa mpweke na mumewe Sajuki, watu wanafuatilia sana maisha yake kiasi kwamba anakosa uhuru.
Alisema, wengine hutafsiri vibaya hata wanaume anaokuwa nao karibu kikazi au marafiki, akafafanua: “Nashangaa kila nitakachofanya kinaanikwa na kuonekana ni kibaya wakati nami ni binadamu ninao uhuru wa kufurahi na kujiachia nitakavyo ili mradi sijavunja maadili.”

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter