ZITTO KABWE AGOMA KUMUOA MTOTO WA RAIS KIKWETE....



Zitto Kabwe amekanusha uvumi ulioenea kuwa anampango  wa  kumuoa mtoto wa Rais Kikwete na ndio maana amepunguza makali yake Bungeni ya kuuliza maswali na kuchangia hoja ...

Zitto alitoa kauli hiyo  juzi wakati akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mpanda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Maridadi....

Alisema uko uvumi ambao umeenea hapa nchini kuwa makali yake yamekupungua bungeni kutokana na yeye kutoka  kimapenzi na  mtoto wa Rais Kikwete wakati sio kweli .

Alifafanua kuwa yeye Bungeni hayuko kwa ajiri ya kupigana ngumi bali yeye siku zote toka amekuwa mbunge amekuwa akipigania kutoa hoja zenye nguvu ndani ya Bunge kama hana hoja za msingi huwa hakulupuki ovyo ovyo

Alieleza ndio maana katika kikao kijacho cha Bunge ameisha wasilisha maombi ya mswada binafsi wa kupendekeza kufutwa kwa sheria ya mwaka 1976 sheria namba 3 ambayo amedai inavinyima haki na uhuru vyombo vya habari ..

Wako viongozi ambao  wamekuwa wakiitumia vibaya sheria hiyo na hasa pale wanapo kuwa wamekosolewa au kuandikwa vibaya na magazeti ...


Alisema kitendo cha kuyafungia magazeti ya Mtanzania na Mwananchi ni ukiukwaji wa katiba kwani kila mwananchi ana haki ya kupata habari na kitendo hicho kinapunguza ajira kwa vijana 
 
Alisema leo hii Serikali inapenda kufanya mambo yake kisiri na ndio maana hata mishahara yetu sisi wabunge ambao mmetuchagua nyinyi wananchi hamuijui wakati ni haki yenu .


Mshahara wa Mbunge kwa mwezi ni Tsh 11,200,000 wakati waziri mkuu anapata mshara wa shilingi milioni 26 kwa mwezi na kila kitu anapata bure .Kama ni kosa kutamka mshahara basi namie nichukuliwe hatua kama magazeti yalivyo fungiwa na kesho nikiwa Wilayani Sikonge ntataja na Rais anapata mshahara kiasi gani kwa mwezi 

Kuhusu katiba aliomba marekebisho ya katiba yazingatie zaidi kuwapa mamlaka ya maamuzi wananchi kuliko viongozi kama ilivyo sasa na alishauri mbunge awe mbunge tuu na asiwe waziri kwani mbunge anapo kuwa waziri matokeo yake ni wananchi waliomchagua kukosa uwakilishi bungeni .. 

Alisema anao mfano hai kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda toka amechaguliwa kuingia Bungeni mwaka 2000 hajawahi kuuliza swali hata moja bungeni kama kuna mtu anaushahidi wa swali lolote ambalo Pinda aliwahi kuuliza yeye Zito yuko tayari kumpa shilingi laki mbili .



Alifafanua kuwa Pinda alichaguliwa kuwa Mbunge kwa mara ya kwanza na aliteuliwa kuwa naibu wa Tamisemi hivyo nafasi hiyo ya uwaziri imembana muda wote .

-Katavi yetu

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter