WASTARA APEWA OFA YA MGUU WA BANDIA...!!



STAA wa filamu za Kibongo, Wastara Juma Jumamosi iliyopita alikwea pipa kuelekea nchini Kenya ambako ana ziara ya siku nne kikazi na akiwa humo alipata fursa ya kupewa mguu wa bandia bure na wenyeji wake huku pia akiahidiwa kufanyiwa ‘check-up’ ya mwili mzima

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Wastara alisema kuwa anajisikia furaha kupewa ofa hiyo kutoka kwa wadau wa tasnia ya filamu pande za Kenya ambao wamekuwa wakivutiwa na kazi zake. “Nimepewa ofa ya mguu bandia wa bure ambao utanisaidia, pia nitafanyiwa uchunguzi wa mwili mzima pamoja na mambo mengine. Nina furaha kwa heshima hiyo niliyopewa na wadau hao na kwa msaada wao huo, Mungu atawalipa,” alisema Wastara. Enzi za uchumba wake na marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ walipata ajali iliyosababisha Wastara kukatwa mguu ambapo aliwekewa wa bandia. hivyo mguu huo aliopewa ni wa pili ili kama atahitaji

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter