DEREVA WA BODA BODA ALIYEFUMANIWA NA MKE WA MTU ASAKWA NA POLISI..!!


MWENDESHA bodaboda ambaye alifumaniwa na mke wa mtu hivi karibuni huko Kigamboni-Kibada, Dar, maarufu kwa jina la Chidi anasakwa kwa udi na uvumba baada ya kuripotiwa kumshushia kipigo mzazi mwenziye aliyejitambulisha kwa jina moja la Husna.
Tukio la kipigo lilitokea Septemba 26, mwaka huu maeneo hayo ya Kibada ambapo chanzo kilibainisha kuwa Chidi alipata wivu wa mapenzi baada ya kusikia tetesi kuwa mzazi mwenzake ametangaza kuwa hana mpenzi kufuatia jamaa huyo kufumaniwa.
Katika kuchimba zaidi tukio hilo, ilidaiwa kuwa Chidi alimtelekeza mwanamke huyo na mtoto wake mdogo aitwaye Adam na kwenda kuishi na mke wa mtu ambaye ndiye aliyeshikwa naye ugoni.
Akizungumza na gazeti hili, Husna alidai kuwa amekuwa akipeleka malalamiko kwa Chidi na ndugu zake kuhusu huduma hafifu kwa mtoto wake lakini mara zote jamaa huyo alikuwa mkali na kufikia hatua ya kutoa fedha kidogo.
“Baadaye nilikuja kugundua kwa nini hatoi fedha ya matumizi baada ya kusoma gazeti lenu (Risasi Mchanganyiko) kuwa Chidi amenaswa ugoni na mke wa mtu.
Alisema tangu Chidi ashikwe ugoni na mke wa mtu, amebadilisha jina na kujiita Supastaa huku akitembea na nakala ya gazeti ambalo lilichapisha habari ya yeye kufumaniwa.
Alisema Husna alipoamua kukaa pembeni ndipo Chidi akamfuata na kumpa kichapo hivyo anasakwa na polisi Kigamboni kwa jalada la kesi namba KBA/RB/549/2013-TAARIFA.


----GPL

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter