Imethibitika rasmi kuwa wakati wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakilalamikia maslahi madogo, mbunge mmoja hulipwa mshahara wa Sh. milioni 11 kwa mwezi.
Kiasi hiki hakijumuishi posho ya Sh. 330,000 anayolipwa mbunge kwa kuhudhuria kikao kimoja kwa siku. Posho ni Sh. 80,000 za kujikimu akiwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao Sh. 200,000 kwa siku na mafuta ya gari Sh. 50,000, jumla kuwa Sh. 330,000 kwa siku.
Aidha, mbunge mmoja hulipwa ‘gratuity’ (kiinua mgongo au bahashishi) ya Sh. milioni 72 baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano cha ubunge.
Aidha, wabunge hupewa fedha za Mfuko wa Jimbo Sh. milioni 30 kila mwaka kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo katika majimbo yao.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....