TAARIFA MUHIMU KUHUSU AFYA YA MZEE SMALL...

Taarifa / Mrejesho : Kwa wote walioguswa na kuumwa kwa nguli wa sanaa za maigizo hapa nchini, Mzee Small, taarifa ni kuwa amepata nafuu na anatembea japo kwa fimbo ingawa mkono wake bado umelemaa. 943108_10151600391149728_1555101358_n Changamoto kubwa kwake ni dawa za kuchua, takribani 30,000/= kwa mwezi pamoja dawa za kusaidia kuyeyusha damu iligundulika kuganda kichwani mwake, takribani 50,000/= kwa mwezi pamoja na mengineyo madogo madogo, ANAWASHUKURU SANA WOTE MNAOGUSWA NA KUMJALI, Kwa msaada wowote tafadhali wasiliana na mkewe, 0658111311.
 
Angalizo; Bi Kidude aliteseka mno na hata nyumba aliyokuwa akiishi kwa muda mrefu ilikuwa pagale, na bila aibu alipofikwa na umauti, Rais wetu wa Serikali ya Mapinduzi aliongoza ujumbe wa Serikali na mengi mazuri yalisemwa juu ya nyota hii iliyoachwa ikaadhirika, NAULIZA TU HIVI MPAKA LINI?????????

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter