1) Mwigulu Vs kesi feki ya Dr Kitila na Mwita Mwikwabe Waitara inayoendelea singida.
Leo nimepata taarifa muhimu ya ushiriki wa Mwigulu Nchemba katika kesi inayomkabili Dr Kitila Mkumbo na Mwita Mwikabwe Waitara. Najua wengi mnakumbuka kuwa Dr Kitila Mkumbo na Mwita M. Waitara walifanya mkutano wa hadhara ktk Jimbo la Mwigulu mwaka jana. Baadaye CCM na serikali wakafungua kesi dhidi ya makada hao wawili wa CHADEMA, wakituhumiwa kumkashifu Mwigulu mwigulu Nchemba. Kesi inaendelea hadi sasa mahakamani, ingawa Mwigulu hajakamatwa wala hajaitwa mahakamani.
Nimepata ushahidi gani leo??
Baada ya mimi na wenzangu kwenye Chama kufuatilia kwa niia zetu tumegundua kwamba kesi zote mbili zilizofunguliwa (Lugha ya matusi dhidi ya Kitila na waitara) na kesi ya mauaji dhidi ya wanachama wengine Singida, zilitengenezwa na Mwigulu Nchemba na zilifunguliwa na Jamhuri kwa maelekezo yake kama ushahidi unavyoonesha hapa chini.
Mosi, vijana waliotumika baadhi yao walitoka Dar es salaam na walikodiwa na Mwigulu Nchemba kwa ahadi ya kupewa PIKI PIKI akiwepo Flavian Njama ambaye ni katibu wa ccm wa kata ya Tandika hapa hapa Dar es salaam na ambaye naye ni mmoja wa washtakiwa Singida. Mpaka sasa Mwigulu Nchemba hajawapa piki piki na ndo maana siri zimeanza kuvuja. Shame on him
.
Kijana Samaria rafiki yake Mwigulu Nchemba ambaye ni katibu wa kata wa CCM jimboni kwa Mwigulu, pamoja na jina lake kutajwa mara nyingi mahakamani lakini bado hajaitwa mahakamani sawa sawa na Mwigulu Nchemba mwenyewe, ambaye naye alipaswa awe ameshatinga mahakamani kwa kuwa yeye ndo mkashifiwa.
Tatu, nina ushahidi wa kutosha kwamba Mwigulu Nchemba ndo anayegharimia kesi hizi kibinafsi na kutokana na kulemewa na gharama sasa anatamani kesi hii iishe haraka.
Nne, kuna ushahidi ambao uko public tayari kwamba Polisi wenyewe akiwepo ocs tayari wameshatoa ushahidi mahakamani kwamba vijana waliohusika ni wanaCCM na kijana aliyeuawa ni mwanaccm, taarifa ambazo ni kinyume na maelezo ya CCM na Mwigulu Nchemba nje na ndani ya Bunge.
NB; kuna tetesi ambazo ninaendelea kuzifuatilia ambazo zinadai kwamba Mwigulu Nchemba anashawishi baadhi ya Viongozi muhimu serikalini ili ama Dr Kitila Mkumbo atimuliwa Chuo kikuu cha Dsm, au aondolewe kwenye ukuu wa idara alionao pale UDSM. Lengo lake anadai ni kuiokoa CCM Iramba 2015, wakati ukweli ni kwamba, yeye anaona kibarua chake kitaoteshwa magugu na Dr Kitila 2015. Je, atafanikiwa?
2) Mwigulu Nchemba Vs John Mnyika. Mwigulu Nchemba alidai kutumiwa meseji ya kutishwa maisha kwa njia ya simu na John Mnyika. Baadaye Mwanausalama wa CHADEMA, Mabere Marando akamwuumbua kwa kunasa taarifa za uwepo mashine (mitambo) za kutengeneza meseji feki iliyonunuliwa kwa mabilioni fedha za walipa kodi wa nchi hii kutoka nje. Kama siyo kunaswa kwa taarifa hiyo ina maana Mnyika angelala Lupango kama Lwakatare kwa kuwa mchakato wa kufungua kesi ulishaanza serikalini
3) Mwigulu Vs Lwakatare. Nimeandika na watu wengi wameandika uhusiano kati ya Mwigulu Nchemba Lodovick Joseph aliyekamatwa pamoja na Lwakatare ikiwepo kumtumia Ths 50,000/=, pamoja na mawasiliano ya mara kwa mara kati ya Ludovick na Mwigulu. Ikumbukwe kwamba, Mwigulu tayari ameshakiri kwamba yeye ndo aliyepeleka CD polisi akidai kupewa na mwanaCHADEMA. Mpaka leo hajasema kada yupi wa CHADEMA alimpa Mwigulu CD ya Lwakatare, Kwa nini huyo kada wa CHADEMA ampelekee Mwigulu CD badala ya kuipeleka polisi, kwanini CD aliyoitangaza tangu dec 2012 iibuliwe march 2013, siku mbili baada ya Kibanda kutekwa. Maswali ni mengi na hayajibiki, na ndo maana kesi imeshafutwa.
4) Mwigulu Vs tuhuma za Kumkimbia Dr Slaa
Kuna watu walimwona Mwigulu Nchemba akiongea na Nyakarungu (kada wa CHADEMA?). Walichozungumza ni siri yao. Wakiwa ktk kuzungumza kwao wakamwona Dr Slaa anapita jirani, wakamkimbia. Aliyewaona akaweka thread JF kuhusu sakata hilo. Mwigulu mwenyewe akaja kukanusha thread hiyo hapa JF, na haya ndiyo maelezo yake yanayonitatiza sana kuhusu uwezowake wa kufikiri.
Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.
A) Mwigulu hakumwona Dr Slaa na hakumkimbia NA hana sababu ya kumkimbia Vs B) kulikuwa na watu wengi tu na Dr Slaa alipita bila attention ya watu.
Linganisha A na B ujue uwezo wa Naibu katibu mkuu wa CCM, yaani hakumwona Dr Slaa na wakati huo huo Dr Slaa alipita bila attention ya watu wengi kwenye tukio hilo hilo moja.
my take;A) Natambua kwamba huu mradi wa CD ya Lwakatare, Kesi ya Mkumbo kitila/Mwita Waitara, Sakata la Mnyika na Ununuzi wa viongozi wa CHADEMA haukuwa mradi wake kibinafsi -- ni mradi wa chama ni mradi wa Nape, Wasira Jack Zoka nk, lakini kwa nini atumike yeye tu kama siyo wanamwona ni mtu rahisi wa kumtumika kwa miradi ya kuokoa chama chao? Mimi ningekuwa Mwigulu ningeshtuka, ningekataa, siwezi kutumika tu.
B) Kwa kuwa steven Wasira alipata kura nyingi kwa ahadi ya kuisambaratisha CHADEMA, na
kwa kuwa mtego wake umeshashindwa, namshauri akawaombe radhi wanaCCM waliompa kura. Au ana Plan B ya kuisambaratisha CHADEMA?
C) Hivi hii habari ya Mwigulu Nchemba kufanya kila atakacho na hakamatwi itakuwa hivi mpaka lini? Kuanzia tuhuma feki dhidi ya Mnyika, CD ya Lwakatare na Kununua watu toka Dar es Saam kwenda kufanya mauaji Singida ktk mikutano ya CHADEMA pamoja na ushahidi wa wazi wa Polisi Mwigulu hajaguswa. Je hali hii mpaka lini?
SOURCE: JF
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....