Simba imetoa tamko hilo baada ya kiungo huyo kutangaza dau la shilingi milioni 150 kwa timu itakayomhitaji ikiwemo Simba kutokana na mkataba wake kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zakari Hans Pope amesema Ngassa bado ana mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo na kudai kushangazwa na taarifa anazozitoa kiungo huyo kuwa mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, kitu ambacho siyo sahihi.
Aliongeza kuwa kama Ngassa anataka fedha nyingine za kumuongezea ni vema akauambia uongozi na siyo kuzungumza kwenye vyombo vya habari.
“Ngassa ni mchezaji halali wa Simba mwenye mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu yetu, kama unakumbuka tulimchukua Azam kwa mkopo kisha tukamuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja,” alisema Hans Pope.
Wakati Hans Pope akitamka hayo, Ngassa amekuwa akisisitiza mara kwa mara kuwa hakusaini mkataba wa ziada klabuni hapo na kudai kuwa atakuwa huru mara baada ya msimu huu kumalizika.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....