MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imepinga vikali taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari kuwa inamshikilia mtumishi wa mahakama hiyo kwa kuiba bangi iliyofikishwa mahakamani hapo kama kielelezo.
"Taarifa ya kamanda wa polisi kuwa bangi imeibiwa mahakamani si ya kweli na imelenga kuichafua mahakama. Mahakama hawajapata kuibiwa. Taarifa hizo si za kweli kabisa".
Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake kaimu msajili wa mahakama kuu Tanzania kanda ya Iringa Godfrey Isaya alisema mahakama inasikitishwa taarifa ya Jeshi la polisi inayoupotosha umma kwa kutoa taarifa ya
uongo bila kufanya uchunguzi.Amesema kungekuwamo kuibwa vielelezo, ilipaswa kuwepo kwa mlalamikaji ambaye ni Mahakama kwenda kufungua kesi polisi.
Tunakanusha vikali kuwepo kwa upotevu wa kielelezo cha bangi katika mahakama hii Exhitibit Room haijavunjwa iko intact... tulikuwa na kielelezo P.3 katika shauri hilo la jinai namba 24/2012 ambayo ni bangi viroba 8 amri ya mahakama ya kuteketeza ilitolewa tarehe 13/2/2013 na bangi hiyo iliteketezwa chini ya uangalizi wa afisa wa jeshi la polisi na kesi hiyo ilikwisha tarehe 13 /2/2013 na mshtakiwa alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela."
Alisema kama ilivyokuwa katika kesi nyingine za jinai, “tunatoa wito kwa jeshi la polisi Iringa kufanya uchunguzi wa kina kuona bangi hiyo imepatikana wapi kwa kuwa sisi hatuhusiki.”
Pia alisema kama kweli mahakama kuna vielelezo vilivyoibwa, basi polisi wangefika kufanya upelelezi hata kuwahoji kama njia ya kuchunguzi .
"Tunalishauri jeshi la polisi kufanya utafiti wa kina kuhusu suala hili kabla ya kutoa taarifa katika vyombo vya habari"
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....