MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza zawadi kwa watu watakaowezesha kukamatwa kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa nchini bila kulipia ushuru au watakaokiuka sheria za nchi.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Kaimu Kamishna wa Idara ya Ushuru na Forodha na Bidhaa wa TRA, Tiagi Masamaki, lenye kichwa cha habari ‘Biashara ya Magendo Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi’, limewatahadharisha wafanyabiashara na wamiliki wa vyombo vya usafiri kuwa watakaokamatwa mali zao zitafilisiwa.
Bila kutaja aina ya zawadi, taarifa hiyo kwa umma pia imesisitiza kwa kuwataka wanachi wote wanaoishi katika maeneo husika watoe taarifa pale wanapoona mali za magendo zinapoteremshwa au kupakiwa katika bandari bubu.
“Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatoa tahadhari na kuwakumbusha wafanyabiashara, wamiliki wa vyombo vya usafiri na watu wanaoishi katika ukanda wa pwani wa mwambao wa Bahari ya Hindu hususan maeneo ya Mbweni, Mlingotini, Ununio, Kawe, Msasani, Kunduchi na Kigamboni, kwamba uingizaji bidhaa nchini bila kulipa kodi ni biashara ya magendo na ni ukiukaji wa sheria ya forodha ya mwaka 2004”, imeainisha taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imebainisha kwamba, biashara ya magendo inaikosesha serikali mapato, kuhatarisha afya za watumiaji na kuleta uwiano usio sahihi wa biashara.
Baadhi ya bidhaa ambazo zinahusishwa zaidi kwenye biashara hiyo ni pamoja na mafuta ya kupikia, mchele, sukari, maziwa ya unga hasa aina ya Nido, betri za tochi na kanga na vitenge.
“Wananchi wote na hasa wa maeneo yaliyotajwa wanaombwa kutoa taarifa pale wanapoona mali za magendo zikiteremshwa kwenye bandari bubu au kupakuliwa na kusafirishwa kwenye vyombo vya usafiri. Mamlaka ya Mapato itatoa zawadi kwa mtoa taarifa atakayewezesha kodi kukombolewa,” imeeleza taarifa hiyo.
Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kipindi kirefu sasa imekuwa ikishutumiwa na wafanyabiashara hususan wanaoingiza bidhaa kutoka nje, kwamba imekuwa ikisababisha mianya ya kuwezesha kuwa na biashara hiyo ya magendo na ongezeko la rushwa dhidi ya wakaguzi wa mizigo inayoingia.

0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....