Waasi wa M23 wamepambana na wanajeshi wa serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC siku moja kabla ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kuwasili katika eneo hilo.
Mapigano ya Jumatano nje ya mji wa Goma yanakuwa siku ya tatu mfululizo ya mapambano kati ya jeshi la Congo na kundi la uasi la M23.
Mashahidi wanasema mzunguko mmoja wa kombora ulitua katika eneo la Ndosho lililo jirani na Goma na kumuuwa mtu mmoja na kuwajeruhi watatu wengine. Hakuna taarifa kuwa upande upi ulirusha kombora hilo.
Bwana Ban aliwasili mji mkuu wa DRC, Kinshasa Jumatano ili kuanza ziara ya siku tatu iliyolenga kuhamasisha amani na maendeleo huko mashariki ya Congo.
Anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila kabla ya kuelekea Goma Alhamis na baadaye kwenda Rwanda na Uganda.
Nchini Msumbiji hapo Jumanne Bwana Ban alitoa wito wa maendeleo ya haraka ya kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa ambacho kiliidhinishwa kupambana na wanamgambo na makundi mengi hai yenye silaha huko mashariki mwa DRC.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kikosi maalumu cha mapigano mwezi Machi baada ya juhudi zilizoshindikana kwa miaka kadhaa za serikali ya DRC kuleta uthabiti huko mashariki hasa katika jimbo la Kivu Kaskazini. Eneo hilo ni makazi ya makundi mengi ya uasi ambayo yanapigana juu ya eneo lenye utajiri wa madini.
ANGALIA VIDEO HAPO CHINI
ini.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....