KAMA HAKUNA NIDHAMU MASHULENI, MATOKEO YATAENDELEA KUFUTWA KILA MWAKA.....!!

Kumekuwa  na   mvutano  mkubwa  kati  ya  wanataaluma  na  wanasiasa  kuhusu  suala  la  elimu  hapa  nchini.....
Wanataaluma  wengi  wanapinga  uamuzi  wa  serikali  kuyafuta  matokeo  ya  kidato  cha nne  kwa  madai  kwamba  hilo  siyo  suluhisho  la  la  tatizo ......


Wasomi  hao  wanadai  kwamba  hiyo  ni  njia  ya  serikali  kujisafisha  kisiasa  na  kukwepa  kujiuzulu  kama  njia  mojawapo  ya  kuwajibika....

Wakitoa  maoni  kwa  nyakati  tofauti, wanataaluma  hao wanaamini  kuwa, upungufu  wa  walimu, mgogoro  ulipo  baina  ya  serikali  na   walimu,  nidhamu  mbovu  shuleni   ( baada  ya  serikali  kuzuia  matumizi  ya  viboko), ukosefu  wa vitabu  na  maktaba  ndo  vitu vya  msingi   ambavyo vimesababisha  ubovu  wa  matokeo......
Miongoni  mwa  wanataaluma  waliopaza  sauti  hadharani  ni  Makamu  mkuu  wa  chuo  cha  Saint Augostine, SAUT....
 
Akiongea  katika kipindi cha Tuongee asubuhi  leo, Makamu mkuu wa chuo cha SAUT Father Charles Kitima amesikika  akilaani  kitendo  cha  serikali  kuyafuta  matokeo   ya  kidato  cha  nne...
Kitima   alisema wanaosema mitihani isahihishwe upya hawana vision ya nchi hii kwani wako Bungeni kupiga madawati na kufundisha watoto matusi na  kwamba  hawana weledi wa kuongoza nchi hii.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter