JINA LA SUGU LAPIGWA 'STOP' KUTUMIKA BUNGENI....!



KATIKA hali iliyoonesha sintofahamu, jina la utani la Mbunge wa Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chadema, Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi ‘Sugu’  lilionekana kumtatiza Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Anne Semamba Makinda.
Ilikuwa wakati Mbilinyi akizungumza kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo ya Mhe. Fenella Mukangara ndipo alipotibua mambo yaliyosababisha spika atatizwe na jina lake la Mbilinyi.
Mhe. Mbilinyi alipofika ukurasa wa nane wa hotuba yake yenye kurasa 54, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Mhe. Godfrey Zambi (CCM) aliomba mwongozo (kuomba mwongozo ni kumtaka anayehutubia kuacha na kurudi kwenye kiti kisha aliyeomba aongee).
Ndipo Spika Makinda alipomtaka Mhe. Mbilinyi akatishe hotuba yake ili Zambi azungumze.
Hata hivyo, Mbilinyi aliendelea kutiririka kwa sekunde kadhaa kabla ya kutii amri ya spika.
Ilimlazimu spika kumwambia tena akisema: “We mheshimiwa Sugu…” kauli iliyoamsha kicheko kwa wabunge huku Sugu mwenyewe akiwa ameondoka kwenye kipaza sauti huku akimwekea spika alama ya vidole viwili inayotumiwa na Chadema.
Mhe. Zambi alitoa hoja kuhusu hotuba ya Sugu kujaa maneno ya uchochezi.
 Spika Makinda kwa uwezo wake aliamua kuliahirisha bunge mpaka saa 10:00 jioni ya siku hiyo akimtaka Sugu kwenda kuondoa maneno yenye uchochezi katika hotuba yake.
Jioni ilipofika, Sugu akapewa nafasi ya kuzungumza ambapo alianza kwa kusema: “Mheshimiwa spika, natamka ndani ya bunge kwamba kuanzia leo jina la Sugu lisitumike.”
Spika akadakia hapo na kusema: “Tena imekuwa afadhali maana mi mwenyewe sijui ni Sugu au Suguru.”
Kauli hiyo ya Spika Makinda ilisababisha wabunge waangue vicheko.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter