Bomu hilo limelipuka wakati waumini wa kanisa hilo wa wakijiandaa na misa ya uzinduzi wa parokia hiyo....
Mpaka sasa haijajulikana idadi kamili ya watu waliojeruhiwa ama kupoteza maisha lakini taarifa za awali zinasema kuwa baadhi ya majeruhi wamekimbizwa hospitali
Chanzo cha mlipuko huo inasemekana kuwa kuna gari ndogo ilifika kanisani hapo na kusimama....
Baadae alishuka mtu aliyekuwa amevalia vazi mithili ya kanzu na kurusha kitu kuelekea kanisani ambacho ndicho kilichosababisha mlipuko huo..
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni balozi wa Vatican nchini Tanzania.Yupo baada ya kunusurika katika mlipuko huo
Hizi ni taarifa za awali tu. Taarifa kamili itawekwa itakapopatikana. Tafadhali endelea kusikiliza Redio Maria Tanzania (inasikika pia online muda huu wakiwa wanatangaza kuhusu tukio hili )
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....