AJINYONGA KWA KAMBA BAADA YA KUMCHOMA MTOTO WAKE KISU CHA SHINGO...!!


WATU wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti jijini Dar es Salaam mmoja kwa kujinyonga baada ya kumchoma mwanae kisu shingoni alidhani kuwa amemuua. Katika tukio la kwanza mkazi wa Kivule Majohe, Emanueli Salagata (45-50) amekutwa chumbani kwake amejinyonga kwa kamba aliyoitundika kwenye dari. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Komba alisema tukio hilo lilitokea juzi.
Alisema Mei 13 mwaka huu huko katika Klabu ya Pamba kwa Mama Zawadi mtu huyo alimchoma kisu shingoni mwanae, George Emanueli (30). Alipelekwa hospitali ya Amana ambako alitibiwa na kuruhusiwa.

Kamanda alisema marehemu aliacha ujumbe kuwa amejinyonga kwa amri yake na kero za watu.

Katika tukio jingine mkazi wa Kimara Dar es Salaam amefariki dunia baada ya kujinyonga chumbani kwake kwa kamba ya manila aliyoitundika kwenye kenchi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema tukio hilo lilitokea juzi.

Alisema sababu za kujinyonga b hazijafahamika na upelelezi unaendelea.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter