Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina lake, wafanyabiashara wengi mkoani humo wamekuwa wakiamini kuwa ili biashara zao zifanikiwe lazima watoa kafara ya kuua watu.
“Siyo bure ile ni kafara na mambo ya kishirikina, haiwezekani watu wafunikwe udongo kwa pamoja pasipo kuwa na dalili zozote za kuanguka kwa kifusi hicho.
“Freemason pia wameingia sana Arusha na wamewateka watu wengi, hivyo matukio kama haya lazima yatokee haswa vifo vya vijana wadogo ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa,” kilisema chanzo hicho.
Aprili 3, mwaka huu ibada ya mazishi ya waathirika wa maporomoko hayo ilifanyika katika Kanisa la Kilutheri, Moshono na ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu kutoka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....