AFISA MWAJIRI FEKI WA JKT ANASWA...!!

Na Issa Manll
TIMU ya mapaparazi wa Global Publishers bado ipo kazini katika oparesheni ya kusafisha jamii kutoka kwenye uovu uliopitiliza, fuatana na Risasi Mchanganyiko ili kukujuza.
Baada ya juzi tu kufanikisha zoezi la kumnasa staa wa filamu Bongo, Irene Uwoya akiwa hotelini na dogo wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, safari hii ikawa zamu ya Benny Mwambola, mkazi wa jijini Dar ambaye ameingia mtegoni baada ya kubambwa na polisi wa Kituo cha Kijitonyama (Mabatini) kwa madai ya kuwatapeli wananchi fedha akijifanya ni Afisa Mwajiri wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


MALALAMIKO YA AWALI
Mwishoni mwa mwaka jana, tabia ya Mwambola ilitua katika dawati la Risasi Mchanganyiko kutoka kwa watu mbalimbali kwamba,  amekuwa  akiwatapeli fedha zao kwa kujifanya ni mwajiri wa jeshi hilo na ana uwezo wa kuwaingiza jeshini.
Timu ya Global ilijipanga na kuanza kumfuatilia kwa karibu jamaa huyo huku ikitoa taarifa katika kituo hicho cha polisi kwa lengo la kupata ushirikiano.
Askari makini wa Mabatini waliahidi kumtia nguvuni afisa feki huyo ambapo hatimaye Jumatatu iliyopita walitimiza ahadi yao hiyo katika eneo la Sayansi, Dar pale walipombamba Mwambola akiwa na vyeti bandia vya Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Asubuhi ya Jumatatu iliyopita, paparazi wetu alipigiwa simu na polisi mmoja (jina tunalo) na kuongea haya:
“Kaka, yule afisa mwajiri feki wa JKT tumemnasa. Kwa akili lakini.”
Paparazi: Wapi?
Polisi: Hapa naniii, siyo mbali sana.
Paparazi: Hebu kata simu nikupigie mimi tuongee vizuri.
Polisi: Usijali kaka, mi si ndiyo nimekupigia! Simu yangu ina vocha,  ni hapa Sayansi.
Paparazi wetu aliwasha pikipiki lake lenye spidi kama gari la mashindano na kufika eneo la Sayansi ambapo alishuhudia jinsi askari hao walivyokuwa wakifanya kazi yao.

AFISA FEKI LAIVU
Mwambola alikutwa akizozana na dada mmoja ambaye alikuwa amepangwa kama mmoja wa wateja waliokuwa wakitafuta ajira kwenye jeshi hilo.
Katika sakata hilo, askari wa doria waliokuwa kizini wakifuatilia sakata hilo walitua na kutega masikio wakijifanya ndiyo wanasikiliza ishu ilivyo.
Afande: (huku akijua ishu) anti, kwani kuna nini?
Anti: Namdai huyu fedha zangu, nimechoshwa na ahadi zake hewa za kupatiwa kazi JKT.
Kauli hiyo iliwafanya maafande hao wamgeukie jamaa na kumuuliza kama ni kweli alichukua fedha za dada huyo, Mwambola alikiri kufanya hivyo.

AFISA FEKI CHINI YA ULINZI
Kufuatia kukiri huko, askari walimweka chini ya ulinzi jamaa na kumpekua katika kabrasha  alilokuwa nalo ambapo walimkuta akiwa na nyaraka mbalimbali alizokuwa akizitumia kuwatapeli watu zikionesha ni za JKT.
Baadhi ya nyaraka hizo ni pamoja na cheti chenye jina la Mwasiti John Kiburungi kilichotolewa na JKT Juni 2007 kuthibitisha kwamba alilitumikia jeshi hilo.
Cheti hicho kilionesha Mwasiti alishiriki katika Operesheni ya Taifa ya Maisha Bora na kimesainiwa na Mkuu wa JKT Tanzania, Meja Jenerali S. Kitundu.
Baada ya polisi kukamilisha zoezi la kumpekua mtuhumiwa huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mabatini kwa ajili ya hatua zaidi.
Dada aliyetapeliwa akizungumza na mwandishi wetu alikiri kuliwa shilingi 50,000 na Mwambola ambaye alimdanganya kwamba yeye ni Afisa Mwajiri wa JKT.
“Huyu kaka ni tapeli kwani aliniambia kama nina ndugu yangu anayetafuta kazi ya ulinzi nimpe 50,000 atapata kazi lakini jambo la kushangaza nilipompa fedha hizo aliingia mitini hadi nilipokutana naye leo,” alisema dada huyo bila kujua mchezo wote kati yake na polisi, paparazi wetu aliujua.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter