
Mara baada ya habari hiyo iliyoshtua wengi kusambaa kama moto wa kifuu, watu mbalimbali waliliambia Amani kuwa hatimaye Diamond amemalizia kukata uzi wa mwisho wa ndoa ya Uwoya aliyofunga na msakata kabumbu, raia wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ mwaka 2009.
Vyanzo mbalimbali vilikiri kuwa ama kweli kamera zetu ni kiboko katika kutafuta ukweli wa jambo kwani ilikuwa ni minong’ono tu kuwa Diamond anatoka na Uwoya ambaye ni mke wa mtu japokuwa hakukuwa na ushahidi, lakini sasa mambo hadharani.
“Hata kama Ndiku (Hamad Ndikumana) alikuwa haamini sasa kila kitu kipo wazi, sidhani kama hapo kuna ndoa tena. Anataka ushahidi gani zaidi ya huo? Habari ya Ijumaa Wikienda imemaliza kila kitu,” alisema rafiki wa karibu wa Uwoya.
Habari zilieleza kuwa hata wasanii wenzao nao walishtushwa na habari hiyo iliyoweka rekodi kwa mwaka huu kwani kila mmoja alikuwa na lake la kusema huku wakimtupia lawama Diamond.
“Dah! Aisee ninyi kiboko! Hivi huyu Diamond anaona raha gani kusambaratisha ndoa ya mwenzake? Alipotembea na akina Wema, Jokate, Wolper, Penny na Aunt Ezekiel haikuwa ishu sana kwa sababu hawakuwa kwenye ndoa. Lakini kwa Uwoya, amefanya kitu kibaya sana.
“Lakini hivi huyo dogo lengo lake ni nini? Au anataka kuwamaliza wote maana ameshapita nao sana na waliobaki ni wale ambao uzuri wao ni wa kumulika na tochi,” alisema staa mkubwa wa filamu wakati akisoma habari hiyo kwenye gazeti la Ijumaa Wikienda.
Habari za kina zilizonaswa na gazeti hili ni kwamba, mara baada ya kupata ukweli juu ya kusalitiwa na mkewe, Ndikumana ambaye alitua Bongo hivi karibuni alitoweka ghafla ikiwa ni siku chache tangu Uwoya alipotamba kurudiana naye na kuanza ukurasa mpya wa ndoa yao iliyokuwa mahututi.
Kupitia gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko toleo namba 996 la Jumatano ya Aprili 3-5, mwaka huu, Uwoya alitangaza kurejea kwa uhai wa ndoa yao huku wakioneshana mahaba kweupe.
Inaaminika kuwa ili kukwepa aibu hiyo baada ya kubumburuka kwa habari ya mkewe na Diamond, ndipo Ndiku aliyekuwa amejaa tele Bongo akatoweka na haijulikani alipo.

Wema Sepetu.
WEMA ANUNAKwa mujibu wa mtu wa karibu wa Wema, baada ya kusambaa kwa habari ya Uwoya kunaswa na Diamond, mwanadada huyo alinuna kwa kuwa wakati alipodai kuporwa mwanamuziki huyo na Jokate, Uwoya alikuwa mstari wa mbele kuponda kuwa jamaa huyo naye ni mwanaume gani huku akimwita Domo.
“Ukweli Wema amenuna maana hakuamini kama Uwoya anaweza kutembea na Diamond,” kilisema chanzo hicho.....
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....