ACHARANGWA MAPANGA KWA KOSA LA WIZI WA NG'OMBE..!!

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Athuman Salum Mkami, mkazi wa Kitongoji cha Lunulo, Kijiji cha Kisemo mkoani Morogoro, amenusurika kifo baada ya kukatwa mapanga na wafugaji.
Tukio hilo lilitokea Machi 30, mwaka huu kijijini hapo ambapo ng’ombe waliingia shambani kwake na kuanza kula mazao yake na alipojaribu kuwafukuza, wenye mifugo hiyo walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa mapanga.
Akizungumza na Uwazi akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivi karibuni, mzee huyo alisema: “Wafugaji hao walinikata kwa mapanga, inauma sana kwani nilichokuwa nakifanya ni kuwaondoa tu ng’ombe hao wasile mazao yangu lakini mwisho nimeambulia kipigo pamoja na kuchukuliwa fedha na silaha yangu aina ya gobore.
“Nilikwenda kuripoti polisi kisha nikaenda kwenye zahanati ya kijijini kwetu ambapo baadaye nilitakiwa kupelekwa Muhimbili.”

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter