Muigizaji wa filamu aliyepo kwenye orodha A kwenye tasnia ya filamu nchini, Rose Ndauka anatarajia kuanzisha kipindi chake cha televisheni alichokipa jina la 'The Family Talk'
Rose amesema dhumuni la kipindi hicho kitakachoandaliwa na kampuni yake ya Ndauka Entertainment ni kuzungumzia masuala mbalimbali ya kifamilia yakiwemo matatizo yanayozikumba.
“Nimechagua kuielimisha jamii kuwaburudisha na vitu vingine, kwahiyo nimeona nikianzisha TV show ambayo itakuwa inahusu familia, inaongelea matatizo ya familia kwa ujumla pia itakuwa ni njia moja ntakuwa nimeweza kuielimisha jamii na inawezekana wakaweza kuburudika kwenye hicho kipindi pia,” amesema Ndauka.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....