Ilielezwa kuwa jamaa huyo aligundulika majira ya saa 11:00 jioni tangu alipoingia saa 3:00 usiku jana yake ambapo alifanikiwa kutoka kwa kuvunja mlango na kutambaa hadi getini na akipiga kelele kuomba msaada kwa wasamaria wema waliotoa taarifa kwa mwandishi wetu na jeshi la polisi.
Akizungumza kwa shida na mwandishi wetu, Lufa alidai kuwa alikuwa akitokea Rufiji kuelekea Shinyanga na kwamba alilazimika kulala mkoani hapa kwa shughuli zake za kibiashara.
“Nilikagua mazingira ya gesti hii nikabaini haikuwa na huduma ya chakula hivyo niliwaomba vijana wale wanioneshe banda la chipsi.
“Mmoja wa vijana wale alinisihi nipumzike kwa kuwa nimechoka akaniambia nimpe fedha akaninunulie chipsi.
“Baada ya kuniletea chipsi niliwakaribisha lakini walikataa kula kwa madai kwamba wameshiba, cha ajabu baada ya kumaliza zile chipsi nililewa na kupoteza fahamu tangu jana usiku, nimezinduka muda huu.
“Nimejitahidi kukagua ndani nimegundua milango yote imefungwa na hakuna mtu, nimejikokota hadi hapa getini na kuomba msaada kwani walinikomba kila kitu zikiwemo fedha zote kiasi cha shilingi laki 2 pamoja na simu.”
Baada ya kupata msaada wa kutolewa getini, jamaa huyo alizimia alipopandishwa kwenye ‘difenda’ la polisi hivyo akakimbizwa katika Hospitali ya Morogoro na kufikishwa akiwa taaban ambapo hadi mwandishi wetu anaondoka hospitalini.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....