
Wakili  wa Lwakatare, Tundu Lisu (kulia) akimuelekeza jambo Mbuge wa Arusha  Mjini, Godbless Lema wakati wakijaribu kuandaa mipango ya dhamana.


Wakili Peter Kibatara akiweka mambo sawa kabla ya kuanza kumtetea Lwakatare.

Wanachama na mashabiki wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili kabla ya kesi kuanza.

Wakili Nyaronyo Kicheere akimuelekeza jambo Godbless Lema baada ya kesi kuahirishwa, kulia ni Tundu Lisu.

Wanachama wa Chadema wakiwa wametawanyika nje ya mahakama baada ya kesi kumalizika.


Mke wa Lwakatare akitahayari baada ya mumewe kunyimwa dhamana.
Mkuu wa kitengo cha usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  Chadema Wilfred Lwakatare leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya  Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka manne ya  ugaidi. 
Lwakatare amepandishwa kizimbanai sambamba na kijana mmoja  aliyefahamika kwa jina la Ludovick Joseph.  Katika kesi hiyo Lwakatare anatetewa  na mawakili watano, Tundu Lisu, Profesa Safari, Nyaronyo Kicheere,  Mabere Marando  na Peter Kibatara



0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....