SNURA: Siyo kweli, mimi ni Mchaga wa Kibosho Sambarai.
ISHU YA WASANII KUJIUZA
Tetesi za kujiuza kwa mapedeshee hasa wasanii wa kike unazichukuliaje? Movic, Dar, 0774424947.
SNURA: Kiukweli hao wanaojiuza nawahurumia kwa sababu wanavyofanya siyo tabia nzuri kwani wao ni kioo cha jamii hivyo tunatakiwa kufanya vitu vizuri vya kuelimisha jamii, kwa nini wajiuze?
HUYU ANAMPA TAHADHARI
Dada Snura napenda unavyojituma katika kazi zako ila kuwa makini na mavazi ya nusu uchi. Ommy, Dar, 0716252571.
SNURA: Asante kwa ushauri wako ila siku hizi nimejirekebisha.
HUYU ANAMFAHAMU VIZURI
Jina lako ni Ashura mimi nakushangaa hilo jina la Snura unasema ndiyo jina lako halisi, uwe unasema jina lako la ukweli. Nakujua ulikuwa unaishi Kiwalani, Kijiwe Samli mama yako anaitwa Doto. Sofia, Dar, 0658340826.
SNURA: Yote hayo ni majina yangu.
ANAMPA USHAURI
Ninachokusharuri Snura achana na majungu, piga kazi hao wanaosema Wema ndiyo aliyekupandisha wewe achana nao kwani Mungu ndiye anayempandisha mtu na siyo binadamu. Catty, Dar, 0656304533.
SNURA: Nashukuru sana kwa ushauri wako.
JE, WAMEMALIZANA NA WEMA?
Snura nakukubali katika sanaa ila nataka kujua vipi wewe na Wema mmemaliza tofauti zenu au bado? Selemani Alifa, Dar, 0718803204.
SNURA: Asante kwa kunikubali, mimi na Wema tumemalizana.
KAZI NYINGINE TOFAUTI NA UIGIZAJI
Snura wewe ni muigizaji bora katika tasnia ya uigizaji, nilitaka nijue tofauti na uigizaji unajishughulisha na nini? Una mpango gani kwa maisha yako ya baadaye wewe na mwanao? Kido Joseph, Dar, 0653691521
SNURA: Ninafanya muziki, kuhusu mpango wa baadaye kuna vitu natafuta, nikivikamilisha nitamrudia Mungu wangu na nitaanza kuimba kaswida.
BIFU LAKE NA SHILOLE
Snura nakukubali kwa kazi yako, vipi mgogoro wako na Shilole umeisha? Usiendekeze bifu fanya kazi. Glory Mushi, Arusha, 0659393927.
SNURA: Mbona sina mgogoro na Shilole?
HUYU ANATAKA KUMJUA KIUNDANI
Dada Snura nakukubali kwa kazi zako nzuri ila nataka kujua wewe ni kabila gani, umezaliwa wapi, una watoto wangapi? Rama, Tanga, 0655200196.
SNURA: Mimi ni Mchaga, nimezaliwa Dar na nina mtoto mmoja.
ETI KAMUIMBA WEMA?
Nakukubali sana kwenye uigizaji mpaka sasa hivi kwenye muziki, Snura inasemekana wimbo wako wa Debe la Vanga umemuimbia aliyekuwa shosti wako, Wema Sepetu je, ni kweli? Jane, Dar, 0655568840.
SNURA: Sijamuimba mtu.
KUHUSU BABA WA MTOTO
Dada Snura kwanza hongera kwa kazi nzuri ya sanaa, eti jamaa uliyezaa naye huyo mtoto anakuja kumdai mtoto wake wewe unamtimua pia unamwambia mtoto siyo wake. Hata jina la baba hukumpa la huyo jamaa, je ni kweli? J. Said, 0718000790.
SNURA: Mwanangu baba yake huwa anakuja kumuangalia kila mara na jina analotumia ni la baba yake anaitwa Talha Kassim.
BIFU LAKE NA WEMA
Nakupongeza dada Snura kwa kazi zako, kwa nini mlianzisha bifu na Wema wakati nyie mlikuwa marafiki wa pete na kidole? Consolata, Mbalizi, 0757867194.
SNURA: Ilitokea tu ila yameshapita.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....