JACK PATRICK WATOTO WAMECHOKA KUKUONA MTUPU!

NI kipindi ambacho sekta ya urembo inakua japo kwa kusuasua Bongo. Leo ngoja nizungumze na modo maarufu Jacqueline Patrick Cliff mwenye hulka ya kujianika utupu kwa asilimia 95 mitandaoni kila kukicha.


Jack ulipata jina uliposhika namba tatu kwenye Miss Ilala na kushiriki Miss Tanzania mwaka 2005/06. Pia uliuza nyago kwenye video ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Albert Magwea ‘Ngwair’ iliyokwenda kwa jina la She Got A Gwain. Kuanzia hapo jina likawa kubwa na ukawa mwanamitindo maarufu Bongo. Ni katika kipindi hicho cha umaarufu ukaolewa na mtoto wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Abdallah Fundikira, Abdulatif kabla ya jamaa huyo kutupwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Keko, Dar akikabiliwa na msala wa kusafirisha mihadarati. Tangu hapo ndoa yenu ilidaiwa kuingia mdudu kwa kuwa wewe hukuwahi kwenda kumuona mumeo mahabusu.
Utambulisho huo unakutosha.
Mara kadhaa Jack uliwahi kuripotiwa kwa picha zisizotazamika kwa watoto na wakubwa. Wiki iliyopita tena ilisambaa picha ukiwa mtupu kwa madai kwamba ni za jarida maarufu. Sawa, wewe ni modo lakini mbona kuna mamodo wengi ndani na nje ya Bongo hawakai utupu kama wewe?
Mara zote picha zako zikisambaa mitandaoni ukiwa ovyo huwa zinaambata na maandishi kutoka kwako kuwa ‘huna tatizo na mtu’ hivyo unajiachia unavyotaka. Sawa, kila mtu ana uhuru wa kufanya mambo yake lakini wewe sasa umezidi.


Ni juzi tu zilisambaa zile zilizokuonesha ukishikwa vibaya kwenye maungo nyeti wakati wa utengenezaji wa video ya Nataka Kulewa ya Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kuna wenye mtazamo kama wako, wanapenda kukusifia mitandaoni kuwa upo ‘seksi’ lakini matunda yake ni nini? Kwa nini wakusifie wewe wasijiweke wao wakiwa utupu? Wakati mwingine si kila anayekupigia makofi anakupongeza. Ukitaka kujua, sikiliza milio ya makofi. Mingine ni ya kukukejeli, irekodi halafu isikilize ukiwa umetulia, utagundua ninachokisema. Ni mfano tu hapa hakuna makofi bali maoni ya kukusifia. Yapime. Utajua ni ya kukuchora.
Wakati unaolewa ulijitetea juu ya suala hilo kuwa jamaa anakuoa wewe na siyo picha na pia anajua vyema kazi yako ya mitindo.




Baadaye pia nilikusikia tena ukitoa utetezi dhaifu kuwa unafanya hivyo ili kupata tenda za matangazo. Mbona hayo matangazo hatuyaoni? Au yanatumika wapi? Kuna mtu aliwahi kudai upigaji wa picha hizo una biashara nyuma yake. Je, ni kweli? Mbali na matangazo yasiyoonekana, hiyo biashara nyingine ni ipi?
Nilichojifunza ni kwamba ukiacha wazazi, hata watoto wamechoshwa na picha zako za utupu. Wanaujua mwili wako kuwa hauna kovu wala kidoti.
Wanajiuliza, wanajifunza nini kutoka kwako kama dada, mke wa mtu au kioo cha jamii. Wamezichoka! For the love of game!

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter