Harakati za Bongo ilipata muda wa kuzungumza na Mussa Issa maarufu kama “Cloud” na iliweza kupiga story mbili tatu kuhusu familia yake ,
HZB: Mambo vip Brother?
Cloud:Safi kabisa karibu sana nyumbani.
HZB: Nafaham kuwa mmejaliwa kupata mototo wa kiume hiv karibuni, hongera sana.
HZB: Mambo vip Brother?
Cloud:Safi kabisa karibu sana nyumbani.
HZB: Nafaham kuwa mmejaliwa kupata mototo wa kiume hiv karibuni, hongera sana.
Cloud: Asante sana ,yupo jembe anaitwa Nabil.
HZB: Vip anandugu zake wengine?
Cloud: Ndiyo ana dada yake mkubwa anaitwa Afrah, ambaye anamiaka 16 na kaka yake mwingine aitwaye Annuary mwenye miaka 8 lakini wote hao sikainao.
HZB: Hao wawili wanakaa wapi?
Cloud: Afrah anaishi Zanzibar kwa mama yake na Annuary yuko Mbezi.
HZB: Vip bado mpo pamoja na mama zao au mmetengana?
Cloud: Hapana bwana siunajua ujana tena, nilizaa nao enzi za ujana kwa sasa kila mmoja anamambo yake.
HZB:Ok, Unajisikiaje kisikia mkeo Cythia kukuletea Nabil?
Cloud: Kwakweli nilifurahi sana, siunajua raha ya ndoa ni watoto kama mungu amejalia.
Cloud na Mke wake Cythia pamoja na mtoto wao Nabil |
HZB: Ni kitu gani kinamfanya Nabil agundue kama baba yupo?
Cloud:Mimi nina sauti yangu moja inamfanya motto wangu agundue kabisa nikiitoa hiyo, lazima afurahi na kujua kuwa mimi nipo ndani.
HZB: Unapokuwa katika kazi zako za uigizaji, ambapo wakati mwingine inakuchukua hata mwezi mzima bila kurudi nyumbani, watoto wanajisikiaje?
Cloud: Mtoto wangu mkubwa yupo Zanzibar na mara nyingi huwa naenda kwa ajili yake na pia ninapo fanya kazi mkoa huuhuu, nakimbia mara kwa mara kumuona kasha narejea kufanya kazi zangu.
HZB: Vip watoto watatu hao wamekutosha au bado unaendelea?
Cloud:|kwakeli bado mungu akijalia nitaongeza wengine.
HZB: Kuna baadhi ya mastaa wanatabia ya kuficha watoto hasa wa nje ya ndoa, unaweza kuwazungumziaje?
Cloud: mimi siwafichi watoto wa nje ya ndoa na ndomaana nimekutajia wote, kuficha watoto ni ulimbukeni, hakuna kitu chenye raha na Baraka kama watoto. Unawezaje kuficha? Wanaofanya hivyo waache mara moja.
HZB: Haya brother nashukuru sana kwa ushirikiano wako.
Cloud: Poa poa, asante na karibu tena siku nyingine.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....