MCHUNGAJI wa Kanisa la Calnel Centre lililopo Uwanja Ndege mjini hapa, Elias Ambakisye (pichani juu) amemuacha mkewe aitwaye Sabina Lameck kwa madai ya ushirikina.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni katika kikao kilichohudhuriwa na familia ya mchungaji huyo, wazee wa kanisa na waandishi wa habari kilichoitishwa na mtumishi huyo wa Mungu.
Habari zaidi kutoka kwa chanzo chetu zinapasha kwamba, mchungaji huyo aliitisha kikao hicho ili wahudhuriaji wamsikie Sabina aliyekuwa mkewe kabla ya kuachana miaka minne iliyopita akitubu mambo ya kishirikina aliyomtendea.
Imedaiwa kuwa, baada ya mama huyo kupewa nafasi ya kutubu alianza kumtuhumu muumini wa kanisa hilo (jina kapuni) kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Ambakisye ambaye ni mumewe wa ndoa.
Habari zinaongeza kuwa, Sabina aliwaeleza wahudhuriaji wa kikao hicho kwamba mwanamke huyo alichukua nguo za mchungaji na za kwake na kuzipeleka kwa kalumanzila zikafanyiwe ndumba ili warudiane na mumewe.
Sabina aliongeza kuwa, jambo la kushangaza ni kwamba baada ya kufanya ushirikina hawajarudiana na mumewe isipokuwa imekuwa kinyume kwani Ambakisye anataka kumuoa muumini huyo.
Kwa upande wake mchungaji huyo, alimtuhumu Sabina kwamba ni mshirikina na kudai aliamua kutengana naye kutokana na tabia hiyo pia kuzaa na mwanaume mwingine kitendo kilichomdhalilisha sana.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....