Washitakiwa hao walioshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wanadaiwa zaidi ya Sh. milioni 148.
Wanadaiwa fedha hizo ambazo walikopa kati ya mwaka 1994 na 2009 na kukubali kurejesha kwa muda ambao walikubaliana na masharti ya bodi hiyo.
Inadaiwa kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 6 C na H cha sheria ya Bodi ya Mikopo namba 9 ya mwaka 2004, inatamka kwamba bodi iliaminiwa kusimamia utaratibu mzima wa kutoa na urejeshaji wa mikopo iliyotolewa na serikali tangu Julai 1994: Kwa mujibu wa kifungu namba 19 cha sheria ya bodi na miongozo yake, inatamka kwamba kila aliyefaidika na mkopo baada ya kukamilisha elimu yake atarejesha mkopo wa Serikali kupitia Bodi. Wadaiwa walikumbushwa kurejesha madeni kupitia vyombo vya habari, lakini walikaa kimya, hivyo bodi inaomba waamuliwe kulipa.
Bodi ya Mikopo inaomba kila mdaiwa alipe fedha alizokopa na adhabu asilimia 10 ya mkopo, alipe fidia kama mahakama itakavyoona inafaa na pia walipe gharama za kesi.
Wadaiwa katika kesi hiyo wanatakiwa kulipa jumla ya Sh. 135,132,275 ambazo ni madeni waliyokopa kwa ajili ya kuwawezesha kupata elimu ya juu na Sh. 13,513,227 ni adhabu ya kuchelewesha malipo.
Walioburutwa mahakamani ni Adam Coresh, Ally Mwenda, Anna Lymo, Hasma Tullango, Catherine Mhina, Clement Kihamia, Dorin Lyatuu, Farida Zuku, Felix Mosha, Flora Peter, Frank Daniel, Harieth Mazengo, Happynes Saria, Hollo Ngeme, Mwanahamisi Abood, Ndebemeye Philipo, Ndeni Anande na Turphina Matereke.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....