JAMANI SINA MUME WALA MCHUMBA....KABULA

Tumewaletea staa wa muziki na filamu za Kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ambaye leo anajibu na kufafanua kile mlichomuuliza, shuka nayo.

Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
HISTORIA KWA UFUPI
Dada Jini Kabula nakukubali kwa kazi zako nzuri, kiufupi nakupa big up, nataka kujua historia yako kwa ufupi. Ramadhan, Tanga, 0717236195
JINI KABULA: Nashukuru sana, kwa kifupi mimi ni mzaliwa wa Mara na kabila langu ni Mjita. Nikisema nielezee historia yangu nitajaza kurasa zote za Ijumaa Wikienda.

YEYE NA BUSHOKE
Bado upo na Bushoke au mmeachana? Gasper , Dar, 0713359435
JINI KABULA: Mimi na Bushoke tutaachana Mungu akipenda siyo binadamu.

KIPAJI NA SKENDO
Jini Kabula wewe ni mzuri lakini mbona huishi katika misingi ya imani yako, Mungu amekupa kipaji kitumie na siyo kuishi kwa skendo. Farhana, Tanga, 0717461100
JINI KABULA: Asante, nitalifanyia kazi hilo.

SKENDO, MAPENZI
Dada upo juu ila punguza skendo, mapenzi weka pembeni, piga kazi kwani ndiyo mpango. Nancy John, Dar,0653878765
JINI KABULA: Asante.

YEYE NA MR CHUZ
Naomba historia yako, kabila lako, umri, je, umeolewa, bado unaendelea na Mr Chuz (Tuesday Kihangala) kiuhusiano? Unaonekana rangi yako ya ngozi ni ‘krimu’ kwa nini usikubali asili ya ngozi yako? Saphia, Mwanza, 0757101142
JINI KABULA: Mimi ni Mjita, nina miaka 26, sijaolewa, Mr Chuz ni bosi wangu, kuhusu rangi ya ngozi yangu, huo ni mtazamo wako.

HAVUTIWI NA ‘VISERENGETI’
Hivi Kabula kwa nini unapenda kutembea na watoto wadogo ‘viserengeti’, una malengo gani ya baadaye? Eddy, Dar, 0716980402
JINI KABULA: Sivutiwi na watoto wadogo, kuhusu malengo, haya ni maisha yangu siwezi kusema hadharani.

MIMBA YA BUSHOKE?
Nakupongeza Jini Kabula kwa kazi nzuri ya sanaa. Hivi ni kweli una mimba ya Bushoke? Julieth Pascal, Mwanza, 0759886923
JINI KABULA: Asante, siwezi kulijibu hilo.

ELIMU
Najivunia kuwa na dada kama wewe lakini napenda kufahamu elimu yako, pia vipi kuhusu matumizi yako ya fedha kwa siku? Frank Sylvery, 0717525067
JINI KABULA: Nina elimu ya kidato cha nne, matumizi kwa siku ni maisha yangu binafsi siwezi kusema natumia shilingi ngapi.

ANAISHI WAPI?
Jini Kabula wewe ni mwanamke mrembo na mwenye mvuto na muonekano wa kipekee, je, kwa sasa unaishi wapi? Jacob Malack, Dar, 0717649895
JINI KABULA: Asante, naishi nyumbani kwetu Mbagala.

ATANGAZIWA NDOA
Miriamu ile shoo ya Dar Live inanisababisha nitangaze ndoa, kama upo freshI tuwasiliane kabla ya mwezi wa sita, shehe aweke ubani. Dr. Mik, Dar, 0712611046
JINI KABULA: Siko tayari kuolewa kwa sasa.

OMBI BINAFSI
Napenda kazi zako pia napenda uwe dada yangu. Chukua namba zangu kama hutajali nitafute. Rajab, Dodoma, 0755827822
JINI KABULA: Nitakutafuta.

ALIPIGWA CHINI?
Jini Kabula nasikia ulikuwa na boyfriend lakini alikupiga chini baada ya Jumba la Dhahabu, akiamini wewe ni jini kweli. Silwimba, Mbeya, 0762185127
JINI KABULA: Siyo kweli.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter