MSANII mwenye maneno ya shombo kwenye tasnia ya maigizo Sintah, amefunguka kuwa anaiombea tasnia hiyo isikumbwe na dudu baya kama HIV na magonjwa ya zinaa, kutokana na tabia iliyopo ndani ya tasnia hiyo ya kuibiana wapenzi na kutoka wenyewe kwa wenyewe.
Kauli ya msanii huyo imekuja ili kuwafungulia mwaka vizuri na uwe wa mafanikio, ambapo alisema kuwa endapo wasanii hao wataendelea na tabia hizo basi kuna madhara makubwa yanaweza kutokea kwani baadhi ya wasanii wanafanya biashara chafu ya kutembea na wanaume wengi kwa lengo la kuendesha maisha.
Alisema kuwa hana nia mbaya na mtu yeyote na hayo ni mawazo ambayo yanaweza kuleta mapinduzi kwa tasnia hiyo ambayo imekuwa ikipewa sifa mbaya kila kukicha.
“Naipenda sana tasnia hii lakini nachukizwa na baadhi ya wasanii ambao hufanya mchezo wa kubadilisha wapenzi kama nguo, na matukio mengi machafu hufanywa na wasanii hasa pale wanapokuwa kwenye bonanza pengine mkoani au kambini,” alidai.
Hata hivyo aliongeza kuwa wapo wasanii wengine ambao hufanya kazi vizuri na hawajishungulishi na ujinga wowote lakini kuna makundi mengine ambayo yapo kwa ajili ya ngono na kuwapotosha wengine.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....