"SHILOLE ANATULIPA TSHS 3,000/= TU! KATIKA KILA SHOW ZAKE.. TUMECHOKA" WACHEZA SHOW WA SHILOLE WALALAMIKA!!

http://dartalk.com/wp-content/uploads/2013/01/wacheza_show_wa_shilole.jpg


WAKATI msanii Shilole akionekana kufanya show za kusisimua, hali imekuwa tofauti kwani wasichana ambao ndiyo wacheza show wake wameanza kutoa ya moyoni kuwa msanii huyo anapata hela nyingine lakini wanacholipwa wao hakifanani na kazi wanayofanya ya kukatika mauno, ambapo siku nyingine hulipwa elfu 10,000 hadi elfu 3000.
Wacheza show hao walifunwa na mtandao huu maeneo ya Kinondoni Mkwajuni, wakitoa story hiyo kwa rafiki zao huku wengine wakitoa machozi kwa kulalamika maisha magumu, wakati wanafanya kazi kubwa ya kumuigizia pesa msanii huyo.

Walivutwa pembeni ili kuzungumza na mwandishi wetu ambapo walishindwa kutaja majina yao, lakini walisikitishwa na kitendo kinachofanywa na boss wao cha kuwalipa pesa kidogo wakati yeye kila show anapokea hela ikiwa ni pamoja na malipo ya wao lakini kwenye kuwalipa mara nyingi huwapa hela ndogo za nauli pekee.

Hatuwezi kuvumilia malipo tunayopewa amabayo ni kwa ajili ya nauli tu, kama mtu anakupa elfu kumi si kwa nauli tu, na sisi tunafanya kazi kubwa ya kukatika mauno mbele za watu lakini malipo tu yanatukatisha tamaa, walisema.
Hata hivyo waliongeza kuwa msanii huyo amekuwa akiwafanyisha kazi muda wote hasa mazoezi huku akisahau kuwa hata wao wanahitaji kujenga maisha yao kama yeye anavyofanya.

Mwandishi wetu alimtafuta Shilole, kwa lengo la kutaka kuzungumza naye, lakini hakuwa tayari kusema chochote, na alipotumiwa sms ili kuonana na mwandishi hakuweza kujibu.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter