INAWEZEKANA yakawa ni mazoea......
Msanii wa filamu bongo, Jackline Wolper, ambaye inadaiwa kuwa ndiye anayewafunika mademu wenzake kwenye tasnia hiyo kwa kumiliki mshiko mrefu, inadaiwa kuwa amekuwa akiwaza ndani ya mwaka huu atampataje bwana wa kumuhonga vitu vya kifahari kama bahati ilivyomdondokea msimu uliopita kutoka kijana mtafutaji Dallas.
Kuvuja kwa siri hii kumekuja siku chache baada ya mwandishi wa dt kufanya mazungumzo na baadhi ya wapambe wa msanii huyo, ambapo mmoja wao alidai kuwa msanii huyo kwa sasa hana mwanaume anayeweza kumpa vitu ya kifahari kama ilivyokuwa msimu uliopita, hata zile misheshe za kutoka hapa na pale zimepungua kutokana na hilo.
“Rafiki yangu bado hajapata mtu bwana najua ungeona kelele za mjini, saivi yupo tu kama hivi hamna mpya” kilidai chanzo.
Pamoja na ishu hiyo kuvuja Wolper aligoma kuzungumzia ishu hii badala yake alidai kuwa hakuna mtu anayejua siri zake na kama kuna mtu anajua basi abaki na hizo alizonazo.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....