"DIAMOND HASHIKIKI KWENYE SHOW.."-AMINI

http://dartalk.com/wp-content/uploads/2013/01/show_ya_diamond.jpg

WAKATI wasanii wengi wakichemsha kwenye show, mkali kutoka THT, Amini, amesema kuwa anamkubali Diamond kwenye upande wa show kwani anavuta mashabiki wengi kuliko msanii mwengine yeyote Tanzania.

Kauli ya msanii huyo aliitoa jana kwenye usiku wa Wasafi ambapo
Diamond alikuwa akipiga show New Maisha Club, ambapo watu wengi waliojitokeza kwa lengo la kuona msanii huyo anafanya nini ndani ya usiku wake.

Amini alisema kuwa kutokana na umati uliojitokeza haamini kama kuna msanii mwingine anayeweza kujaza club hiyo kama alivyofanya
Diamond kwani watu walikosa sehemu ya kukaa huku wengine wakiishia kubaki nje.

“Hapana watu ni wengi sana na naamini Diamond kwa sasa kwenye upande wa show yuko safi sikutarajia kama watu wanaweza kujaa kiasi hiki, na si hapa show zake nyingi jamaa anafanya poa namkubali sana,”
alisema.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter