Sasa umeibuka mtindo kwa kila msanii anayejiona staa kutangaza dau analotaka kulipwa katika filamu wakati wengine hajawafikia hatua hata ya kuitwa ‘Professional Actor/Actress’ au kufikia kiwango cha kujulikana hata Afrika Mashariki.
Msanii huyo aliongea na mtandao Huu katika mahojiano mafupi ndipo aliposema kuwa huwa anakaa na kuwaza ni kitu gani kitakachomfanya alipwe pesa nyingi katika kila filamu anayocheza na jibu ambalo huwa analipata ni kuongeza ubunifu katika kazi anazofanya.
Alisema kuwa wasanii wanaotangaza kutaka kulipwa kiasi fulani cha pesa ni wale ambao wanajiona mastaa kwa sababu ya kutokea kila siku kwenye vyombo vya habari huku wengine wakitokea kwa mambo ya ajabu basi tayari wanajiweka kwenye ubora wa hali ya juu.
Aliongeza kuwa ameshacheza filamu nyingi na zote zimempa umaarufu ikiwemo ‘Lovers Island’ na nyingine kibao lakini hajafikilia hatua ya kutangaza dau la kulipwa kwani anaamini waandaaji watamtumia kwenye filamu zao kutokana na kiwango chake na si urembo wake au kujulikana kwa sababu ya skendo.
“Mara nyingi huwa napenda kujituma kwa sababu hiyo ndiyo njia ambayo itanifanya mimi niweze kulipwa pesa nyingi katika kila filamu ninazofanya, na sidhani kama nikijulikana sana kwa kupitia skendo ndo naweza kubadilisha maisha yangu na kutaka nilipwe kiasi fulani au kwa sababu ya uzuri, nitalipwa kulingana na kiwango changu kwenye kazi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....