KUMBUKUMBU YA SHARO MILIONEA YAANDALIWA,ITAFANYIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA AMBAYO PIA NDIO SIKU ALIYOFARIKI DUNIA...

Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’.
IKIWA anakaribia kufikisha mwaka mmoja tangu afariki dunia, marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’, dua maalumu ya kumbukumbu inatarajiwa kusomwa Novemba 26, mwaka huu.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni jijini Dar es Salaam, mchekeshaji wa kike, Sherry Magali, alisema ameandaa dua itakayosomwa nyumbani kwake Mabibo, Dar siku hiyo kwa sababu pia ni siku yake ya kuzaliwa.
“Mimi na Sharo tunashea siku ya kuzaliwa. Sharo amefariki siku yake ya kuzaliwa, kwangu mimi nimeona ni vyema kufanya dua hii muhimu kwa lengo la kumkumbuka mwenzetu,” alisema Sherry.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter