- Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa
kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa
wa Mwanza ameuawa na genge
ndani ya Polisi akiwemp Kamanda
Polisi anayejulikana kwa jina la
Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti
katika ukurasa wa Mbele kabisa
Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana
na mmoja wa jambazi sugu
ajulikanaye kwa jina la Edward
Malele kujisalimisha ktk vyombo
vya ulinzi na kutoa siri zote.
Jambazi huyu aliombwa wa genge
ndani ya polisi kushiriki katika
mpango wa kumwua kamanda
Barlow. Akakataa kwa kuwa
aliwahi kumfahamu kwa karibu
kamanda Barlow.
Baada ya kukataa kutekeleza agizo
hilo baada ya siku chache
alishtakiwa kwa kosa la ujambazi
na kuswekwa Rumande.
Akiwa huko ndani ya wiki moja
alisikia habari za kifo cha
kamanda Barlow. Akajua akina na
Muna aliowakatalia wamefanya
kazi aliyoikataa yeye. Na alijua
yuko mahabusu kwa sababu ya
kukataa mradi huo.
Baada ya kukaa huko muda mrefu
bila shitaka kueleweka wala
mshataki wake huko Lupango
walimua kumwaichia. Akagoma
kutoka kwa sababu anajua kuwa,
kwa kuwa amepelekwa huko ili
kuficha siri hivyo, akitoka lazima
atauawa. Baada ya muda akaamua
kukubali kutoka lupango na
kukimbilia kituo cha JWTZ huko
Mwanza.
Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha
na wanajeshi walimwonea huruma
wakampa Tsh 100,000/= ilie aende
Bungeni huku wakiwa
wamemkabidhi namba za simu za
wabunge 2 wa upinzani ili
wamsaidie.
Kutokana na kutokuelewa kwake
alipokuwa anashangaa shangaa
katika eneo la Bunge, alikamatwa
na polisi wanalinda eneo hilo.
- Polisi hao wakapiga simu Dodoma
haraka mwanza wakataka
arudishwe mwanza kwa kuwa ni
jambazi sugu.
Hata hivyo, kwa katika
kurupushani hiyo taarifa
zimeshameshamfikia Pinda na
Nchimbi ambapo gazeti linaripoti
kuwa Pinda ameagiza kijana huyo
apewe ulinzi na asirudishwe
mwanza.
Hata hivyo amepelekwa kusiko
julikana.
Kwa mapana zaidi soma gazeti la
Jamhuri hata hvyo linanunuliwa kwa
kasi na watu wasiofahamika.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....