PICHA: MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI NASSARI AKICHANGIA DAMU KWA MAJERUHI WA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA...!!


 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Akitoa Damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa mlipuko wa bomu Leo jijini Arusha. 


Nassari Akitoa damu kwa Majeruhi  Mlipuko wa BomuMbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari mbali ya kuwahamasisha watu kutoa damu, pia hivi punde amemaliza kutoa damu kwa ajili ya kuwachangia majeruhi waliolipukiwa na bomu kanisani LEO. Pichani Nassari akionekana akitoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi.Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari LEO tangu majira ya saa 5:30 asubuhi wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahamasisha watu kutoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi mbalimbali waliojeruhiwa na bomu katika kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti mjini humo.Kutokana watu wengi kupoteza damu na kumwagika kwa wingi. Mbali na hilo baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo wameueleza mtandao wa Habarimasai.com kwamba hivi sasa wana wakati mgumu katika kufanya usafi na mwandishi wetu Joseph Pantaleo ameshuhudia manesi hao wakisafisha damu sakafuni kila wakati huku wakimwaga maji na dawa ili kuondoa mabaki ya damu hiyo.Lema na Nassari wameonekana wakiwahamisisha watu kutoa damu na wengi wameitikia wito huo. Endelea kusoma habarimasai.com kwa taarifa mbalimbali zaidi.

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter