Leo tunashuhudia mwendelezo wa serikali kushinikiza kuwaondoa wananchi wa Loliondo ili kupanua kitalu cha uwindaji kwa mwarabu ambaye kipande alichopewa kimeshamalizika wanyama na anataka ZAIDI. Kinachotia mashaka ni namna ambavyo mwekezaji huyo alivyoweza kujijengea himaya yake ambapo hata mtu anapokaribia ama kuingia eneo lile anakutana na ujumbe KARIBU KATIKA FALME YA NCHI ZA KIARABU ambapo kwa ujumbe huo ni dhahiri kipande ile ni milki ya mfalme wa uarabuni.
Katiba imekiukwa na wanaotakiwa kuijibu hii ni IKULU kwa sababu ndiyo tuliowapa mamlaka ya kuilinda Katiba chini ya Rais. Nanukuu hapa chini kipengele kilichokiukwa, soma kwenye bold
28. Ulinzi wa taifa Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6 (1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.
(2) Bunge laweza kutunga Sheria zinazofaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinzi wa taifa. (3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi, wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa, hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.
(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Nchi imemegwa na kupewa asiyestahili. Nini kifanyike?
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....