Lugha kama hizi zimesababisha Watanzania wengi wakose hamu ya kusikiliza vikao vya Bunge.
Tumechoshwa na lugha chafu za waheshimiwa. Bunge ni sehemu ambayo tulipaswa kuwa tunasikiliza hoja za sera zikiwasilishwa na sheria kutungwa, lakini imeshindikana.
JOSEPH MBILINYI:
"Mambo mengi ya nchi hii hayaendi kutokana na SERIKALI PUMBAVU....
Hatuwezi kuwa na WAZIRI WA ELIMU BOYA mwenye elimu ya kuunga unga halafu tufanye vizuri katika sekta ya elimu , haiwezekani."
LIVINGSTONE LUSINDE:
"Siwezi kuikubali taarifa hiyo.Nadhani huyu mtu bado amechanganyikiwa na uchaguzi wa kenya.Mimi sijaitaja Chadema bali nimesema kuna chama kimoja cha siasa,SIJUI YEYE ANAWASHWA NINI..!!
JUMA NKAMIA:
Sugu naomba unyamaze.Mimi ndiye nazungumza.Mimi siongei na mbwa,naongea na mwenye mbwa.
Khatibu Saidi Haji (Konde - CUF)
Alimtukana Freeman Mbowe mbunge wa Hai kwa kusema "Mbowe kaja hapa anajambajamba tu" akilalamikia hoja ya Mbowe kuhusu idadi ya watu wa visiwani. Alimtukana Mchungaji Msigwa: "Wewe Msigwa ni mchungaji wa watu au mchungaji wa nguruwe? "Alitoa tusi hilo kutokana na Mchungaji Msigwa kutoa kauli ya kwamba Zanzibar kuna udini.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....