NGULI wa filamu za Kibongo, Mohammed Fungafunga ‘Jengua’ amewafungukia baadhi ya wasanii wa kike wanaofanya filamu za nusu uchi kuwa zinawaharibia soko la tasnia hiyo kwani wakati mwingine wazazi hushindwa kununua kuhofia kuangaliwa na watoto wao.
Akizungumza na Risasi , Jengua alisema kuna baadhi ya wasanii wameshazoeleka kwa filamu hizo kiasi kwamba wazazi wanachenga kuzinunua ili kutowaharibu watoto wao.
“Hivi jamani hutuwezi kutengeneza filamu bila kuweka hayo mambo ya utupu? Mbona sisi wazee tunacheza filamu bila kuwa na huo utupu lakini bado tunaendelea kuwa na mashabiki wengi na filamu zetu zinanunuliwa? Tukiendelea hivi tusishangae pale ambapo filamu zetu zitadunda sokoni,’’ alisema Jengua.

0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....