Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema “mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
Katika sentensi nyingine, Mbaula anasema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza 42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....