Breaking Newzzzzzzzz:Mbunge wa Chambani Salim Hemed Khamis,afariki dunia mchana huu.


Pichani ni Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba Mbunge wa Chambani,Bwa.SalimHemed Khamis,mara baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu ya haraka.
=======  ======  ======
Habari  zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde inaelezwa kuwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chambani-Pemba, Salim Hemed Khamis,ambaye hapo jana alianguka ghafla jijini Dar Es Salaam alipokuwa akihudhuria vikao vya kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali hiyo ya Taifa ya Muhimbili,aidha chanzo cha habari hizi kimeongeza kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.Tutazidi kuwafahamisha zaidi kadiri ya habari zitakavyokuwa zikiingia.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi-Amin

Tupe maoni yako hapo chini..!

Share this article :

'LIKE' UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI...!

0 comments:

Post a Comment

TOA MAONI YAKO HAPA....

 

Copyright © 2010 GUMZO LA JIJI.

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter