P Funk Majani amewapa makavu watu wanaochonga kuhusu maendeleo yake hususani wale wote ambao wanapiga majungu kuwa mkali huyo amepotezwa na vijana wadogo kwenye industry ya mziki.
“Kuna watoto wadogo siku hizi wanakurupuka wanajiona wao ndio wao, juzi kati nikiwa kwenye club moja nasikia kiproducer kinachonga kuhusu mimi kenyewe kana sijui nyimbo moja au tatu zimehit mimi nina nyimbo zaidi ya 100 ambazo zimehit na hadi akina Mhe Mkapa enzi hizo, wametukubali we utaniambia nini” P funk alinena.
Majani amefunguka kuwa kuna watu wanamtafuta chuki ili kumpachika skendo akitolea mfano msanii wa kizazi kipya Ney wa Mitego kuwa haelewi kitendo cha rapper huyo kumtukana kwenye nyimbo yake kulikua na lengo gani kwasababu msanii huyo hamkaribii hata kidogo kwa level zake.
0 comments:
Post a Comment
TOA MAONI YAKO HAPA....